VIWANGO VYA FIFA: ARGENTINA KINARA DUNIANI, SENEGAL YAONGOZA AFRIKA
Taifa
la Guinea-Bissau ndio taifa lililofaidika sana katika orodha mpya ya shirikisho
la soka duniani Fifa mwaka 2016 baada ya kupanda nafasi 78 tangu Disemba mwaka
uliopita.
Taifa
hilo sasa limeorodheshwa la 68 katika orodha ya dunia na la 15 barani Afrika.
Hatua
hiyo inamaanisha kwamba Guinea Bissau ipo juu ya mataifa ya Uganda ,Togo na
Zimbabwe ambayo pia yamefuzu katika kombe la mataifa ya Afrika nchini Gabon.
Senegal
inakamilisha mwaka huu ikiwa ndio taifa linaloongoza barani Afrika na nambari
33 duniani.
Guinea
Bissau ilifuzu katika michuano ya mataifa ya Afrika baada ya kuishinda Kenya na
Zambia mwaka 2016.
Walipoteza
mechi yao ya mwisho dhidi ya Congo-Brazaville lakini ikafanikiwa kumaliza
katika kilele cha jedwali ili kuweza kufuzu Gabon.
Katika
orodha ya dunia Argentina bado inasalia katika nafasi ya kwanza.
Orodha
ya mataifa ya Afrika duniani:
Senegal
(33)
Ivory
Coast (34)
Tunisia
(35)
Egypt
(36)
Algeria
(38)
DR
Congo(48)
Burkina
Faso (50)
Nigeria
(51) (hakufuzu Gabon 2017)
Ghana
(53)
Morocco
(57)
No comments