MHE HAPI AISHIKA PABAYA ZANTEL, YALIPA DENI LA ZAIDI YA MILIONI 687 NDANI YA SIKU 7 ILIZOAGIZA
KAMPUNI
ya simu za mkononi ya Zantel Tanzania imelipa zaidi ya Sh milioni 687 baada ya
kupewa siku saba na halmashauri hiyo iwe imelipa fedha hizo ambazo zilikuwa za
kodi ya pango inazodaiwa na manispaa hiyo.
Fedha
hizo zililipwa Desemba 21 na mkataba huo wa zamani unaisha Januari mwakani
ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema wanaandaa mpya wenye
viwango vya malipo vya sasa.
Aidha
halmashauri hiyo imeamua kuelekeza fedha hizo ambayo ni sh 687,931,040 katika
ujenzi wa vyumba vya madarasa 40 katika halmashauri hiyo kwamba kama itaonekana
inawezekana kujenga shule nyingine mpya ya sekondari.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Hapi alisema fedha hizo
zimelipwa baada ofisi yake kubaini mchezo mchafu uliokuwa umefanywa na
watendaji wa halmashauri yake waliokuwepo huko nyuma ambao walificha mkataba
kati yake na Zantel.
Aidha
aliipongeza Zantel kwa kutii maagizo waliyopewa na kulipa fedha hizo na tayari
wamepewa risiti kuonesha kupokea fedha hizo na kwamba watu wote waliohusika
katika jambo hilo watachukuliwa hatua za kisheria.
Alisema
baada ya malipo hayo, ameelekeza Manispaa kutumia fedha zote hizo kujenga
vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo.
“Takwimu
zinaonesha mwaka huu watoto 19,000 walifaulu katika Halmashauri ya Kinondoni
waliochaguli kujiunga na Sekondari ni 12,889 na hadi sasa wanafunzi 3,169
hawajapata nafasi katika shule zetu kwasababu ya ufinyu wa madarasa,” alisema Hapi
No comments