KAMANDA MPINGA: MARUFUKU POLISI KUVISHA MABANGO MADEREVA WALEVI
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema wamesitisha
kuwatangaza watuhumiwa katika mitandao ya kijamii baada ya kupata malalamiko ya Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora.
Hata
hivyo, amesema hadi wanasitisha walikuwa wamewakamata madereva 20 wa Dar es Salaam, lengo likiwa ni
kuonyesha jamii ili wengine wenye tabia hiyo wajifunze kupitia kwa wenzao na
kuacha kuendesha wakiwa wamelewa.
“Kwa
sababu watu wengi wapo mtandaoni ilikuwa rahisi ujumbe kuwafikia kwa wakati
mmoja. Tulipata malalamiko ya haki za binadamu kuwa kufanya hivyo
kunawasababishia kudhalilika katika familia zao, tukaona tusitishe,” amesema
Mpinga.
Hata
hivyo, amesema pamoja na kusitisha utaratibu huo, madereva wasijisahau kwa
sababu vijana wapo kazini na wanaendelea kuwakamata wale wote watakaokiuka
sheria za barabarani, ikiwamo hiyo ya kuendesha wakiwa wamelewa.
Awali,
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imelitaka Jeshi la Polisi, Kikosi cha
Usalama Barabarani, kuacha kuziweka hadharani picha za madereva wanaotuhumiwa
kukiuka sheria, badala yake liwafikishe mahakamani kwanza.
Kauli
ya Tume hiyo imetokana na utaratibu ulioanzishwa na trafiki wa kuwavisha
mabango madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria ambayo yameandikwa makosa yao na
kurushwa kwenye mitandao ya kijamii kabla hawajafikishwa mahakamani.
Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga amesema hayo wakati akifafanua kuhusu kusitisha
kuwaanika katika mitandao ya kijamii madereva wanaokamatwa na trafiki kwa
makosa ya usalama barabarani ikiwamo ulevi
|
No comments