DKT ABASS: SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA BLOGGERS KATIKA KUTOA HABARI PAMOJA NA KUELIMISHA JAMII.
Mkurugenzi wa Habari Maelezo Hassan Abass akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa waandishi wa habari kwa mitandao/bloggers wa chama pamoja na mafunzo.
|
Kaimu mwenyekiti wa muda wa chama cha Bloggers Tanzania Joachim Mushi (aliyesimama) akifafanua jambo katika mbele ya washiriki awapo pichani katika mkutano mkuu wa mwaka wa wamiliki wa blogger, (kushoto aliyekaa) Mkurugenzi wa Habari Maelezo Hassan Abass wakati wa kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama.
Mmoja kati ya waanzilishi wa mtandao wa jamii forums Maxence Melo akiwasilisha mada juu ya changamoto zilizopo katika mitandao ya kijamii hususani Uendeshaji wake pamoja na Uandishi wa habari za mitandao//Bloggers.
Samwel Malecela (Le Mutuz Nation) mmiliki wa mtandao wa wananchi blog akichangia mada kuhusu changamoto ya utoaji wa habari katika taasisi za serikali na idara zake kwa bloggers.
Washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa bloggers wakifatilia mada iliokuwa ikiwasil;ishwa na Maxence Melo juu ya uendeshaji wa mitandao hiyo pamoja na namna ambavyo wanavyotakiwa kuiendesha ili kuweza kuwavutia wasomaji wengi zaidi.
Na frank wandiba
Chama cha wamiliki wa bloggera nchini Tanzania wamefanya mkutano mkuu wa mwaka 2016 wenye lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu mitandao ya kijamii, uendeshaji na uandishi katika mitandao kwa ujumla.
Katika mkutano huo ambao mgeni rasmi aliyefungua mafunzo hayo ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam na mkurugenzi kutoka Habari Maelezo Dkt Hassan Abass ambaye amesema kuwa bloggers ni chombo rasmi cha habari kama vilivyo vyombo vingine vya habari na watu zaidi ya bilioni 3.5 duniani wanalishwa habari kwa sehemu kubwa kupitia chombo hiki.
Pia amesema ili habari iweze kuwafikia jamii kwa haraka, mara nyingi wanatumia waandishi wa mitandao (bloggers) kwani ni chombo cha habari namba moja, hivyo ameongeza kuwa serikali kwa sasa inatambua waandishi kwa njia ya mtandao.
Amewataka bloggers kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya habari, kwa ukweli na usahihi, huku wakitabua kuwa bado wanachokiandika kinaleta manufaa kwa jamii nzima na ndipo jamii itaendelea kuwaheshimu zaidi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa muda wa chama cha bloggers nchini Tanzania Joakimu Mushi amesema kauli mbiu ya mkutano huo ambayo ni ”mitandao ya kijamii ni ajira itumike kwa manufaa” amewataka wanachama wote kuweza kujikita kutoa habari na kujikita kutambua chama kama sehemu ya nafasi katika utendaji wa kila siku.
Dkt. Hassan Abass amesema; “kuanzia sasa chombo chochote cha habari hususani magazeti yanapotumia picha hama habari iliyotoka kwenye mtandao wa kijamii kama (blogs) pasipo idhini ya mwenye mamlaka nayo kusitisha mara moja hama sheria ya hakimiliki itatumika.”
No comments