AMUUA MWENZIE KISA WIVU WA PENZI LA BIBI WA MIAKA 60
KIJANA mwenye umri wa 23 na
mpenzi wake, bibi mwenye umri wa miaka 60 , wakazi wa kijiji cha Tentula, Kata
ya Ikozi wilayani Sumbawanga, wanashikiliwa na polisi wakihutumiwa kumshambulia
na kumuua kikatili jirani yao aitwae Desder Justino (23) kwa kile kinachoelezwa
kuwa ni wivu wa mapenzi.
Inaelezwa kuwa, Justino pia
alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na bibi huyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mauaji hayo
yalitokea Desemba 21 mwaka huu saa nne asubuhi katika nyumba ya mwanamke huyo
iliyopo kijijini Tentula.
Taarifa kutoka kijijini humo
zinadai kuwa, mwanamke huyo licha ya umri wake kuwa mkubwa, alikuwa na uhusiano
wa kimapenzi na vijana hao wawili wa rika moja.
Kamanda Kyando hakuwa tayari
kutaja majina ya wapenzi hao ambao ni watuhumiwa wa mauaji kwa sababu za
uchunguzi.
Lakini alisema mwanaume ana
umri wa miaka 23 huku mpenzi wake ana umri wa miaka 60. Akielezea zaidi,
Kamanda Kyando alisema siku ya tukio Justino alikwenda nyumbani kwa mwanamke
huyo ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi na kumkuta kijana mwingine
(mtuhumiwa), na hapo ndipo ugomvi ukaibuka baina ya vijana hao.Alisema Justino
alijeruwa kichwani.
“Wawili hao yaani wapenzi hao
(mwanamke na mwanaume) walimshambulia Justino (Desder) kwa kumpiga kichwani na
kitu chenye ncha kali na kumjeruhi vibaya na alikufa akiwa anatibiwa
hospitalini,”alisema Kamanda Kyando na kuongeza kuwa, watuhumiwa hao
wanashikiliwa na watafikishwa mahakamani uchunguzi wa awali utakapokamilika.
|
No comments