ALIYEMKASHIFU MTUME MUHAMMAD NA TAARIFA HIYO KUSAMBAA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII AKAMATWA ZANZIBAR
JESHI
la Polisi Zanzibar linatarajia kumfikisha mahakamani mtu anayedaiwa kumkashifu
Mtume Muhammad (S.A.W).
Mtuhumiwa
huyo, Dk. Abdallah Saleh Abdallah (50), mkazi wa Kikwajuni mjini Unguja, baada
ya kutoa maneno hayo ya kashfa juzi na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Unguja, Kamishna wa Jeshi la Polisi visiwani hapa,
Hamdan Omar Makame, alisema walimtia mbaroni daktari huyo wa binadamu baada ya
taarifa zake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwamo wa Facebook.
Mtuhumiwa
huyo anadaiwa kumkashifu Mtume Muhamad na waumini wa dini ya Kiislamu.
“Tumemkamata
mtuhumiwa na tayari tumeshakamilisha kila kitu, ikiwamo taarifa za upelelelezi.
Hivyo kilichobaki ni kumfikisha makahamani tu ili aweze kujibu mashtaka yake,”
alisema Kamishna Makame.
Akiongezea
kuhusu ukusanyaji wa taarifa za upelelezi, alisema wamelazimika kumshikilia
kijana Ali Juma Makame (30) mkazi wa Michenzani mjini hapa ambaye anatuhumiwa
kusambaza video hizo mitandaoni.
“Tunawanasihi
waumini wa dini ya Kiislamu kutokubali kuyumbishwa na kufanya maandamano kwani
kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sheria, ni bora kujiepusha na jambo hili
kwani tayari vyombo vya ulinzi vimeshachukua hatua kwa mujibu wa sheria,”
alisema.
Kutokana
na video hiyo, taasisi mbalimbali za dini ikiwamo Jumuia ya Maimamu Zanzibar
(JUMAZA) na Ofisi ya Mufti, zimelaani tukio hilo na kutoa wito vyombo vya
sheria kuchukua hatua na kufanya kazi bila upendeleo.
Chanzo-Mtanda
blog
No comments