UBALOZI WA MAREKANI NCHINI KENYA WAFUNGWA BAADA YA MTU MMOJA KUUAWA KWA RISASI NJE YA UBALOZI HUO
Jeshi la Polisi jijini Nairobi nchini Kenya linafanya uchunguzi kuweza kubaini kama mtu mmoja aliyeuawa jana karibu na ubalozi wa Marekani alikuwa amekula njama za kushirikiana na watu wengine kufanya shambulio.
Mtu huyo (24) aliuawa jana asubuhi nje ya ubalozi wa Marekani Nairobi baada ya kumshambulia mlinzi kwa kumchoma na kisu tumboni ndipo Afisa mwingine wa Polisi akampiga risasi kichwani.

Maafisa
watano wa FBI na maafisa wa Polisi nchini Kenya walikuwa karibu na eneo
la tukio ambapo ni nje kidogo ya ubalozi wa Marekani.
No comments