SHEKH MUHAMAMAD ABDI, WATANZANIA KEMEENI MAOVU, DHURUMA KUMUENZI IMAM HUSSEIN
Naibu kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasharia Tanzania Sheikh Muhammad Abdi akizngumza na wanahabari Leo Jijini Dar es salaam
Watanzania wametakiwa kuhakikisha
kuwa wanaishi katika njia za kumpendeza mwenyezi mungu ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha maswala ya kuboresha hali ya jamii yanayopewa kipaumbele,kukataa
kudhulumu,kuamrisha mema pamoja na kukemea maovu kama mauaji ya walemavu wa
ngozi,matendo ya kijambazi,ubakaji,ikiwa ni njia ya kumuenzi Imam Hussein
aliyekuwa mstari wa mbele katika kukemea mambo hayo.
Kiongozi huyo amesema
kuwa Imam Hussein ambaye wanamkumbuka leo ni moja kati ya viongozi wa dini
ambao aliwafunza watu namna ya kupinga ukandamizaji,dhuluma katika jamii pamoja
na kutetea haki za wanyonge hivyo ni wakati wa wananchi wa Tanzania kuanza
kufwata maneno yake na kuhakikisha kuwa wanaenzi yale mema aliyoyaacha katika
jamii.
Wito huo umetolewa leo
Jijini Dar es salaam na Naibu kiongozi mkuu wa waislam Shia Ithnasharia
Tanzania Sheikh Muhammad Abdi alipokuwa anazungumza na wanahabari kuhusu
kuukaribisha mwaka mpya wa kiislam mwaka ambao ni wa 1438H katika kalenda ya
kiislam pamoja na kumbukumbu ya Imam Hussein mkutano ambao umefanyika katika
msikiti wao uliopo Kigogo Post Jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa leo hii
dunia inalazimika kuitika wito wa Imam Hussein ili kuinusuru dunia iliyotapakaa
damu kila kona,ambapo akitolea mfano wa mashariki ya kati ambapo imekuwa
ikishughudiwa watoto wanavyochinjwa na maelfu kukimbia makazi yao kwa sababu ya
uharibifu,huku pia katika bara la Africa ikishughudiwa makundi ya kiigaidi
yakiibuka katika nchi nyingi ambapo yamekuwa yakileta madhara makubwa kwa
wananchi wasio na hatia huku akisema
kuwa mambo haya ni mambo ambayo yalikuwa yanamkera sana Imam Hussein na kama
angekuwepo angejitokeza kupambana nayo.
Aidha Sheikh Muhammad
Abdi ameonyesha kuhuzunishwa na baadhi ya matendo ambayo yamekuwa yakitokea
nchini Tanzania yakiashiria matendo ya kigaidi na mauaji kwa wasio na hatia
ambapo ametoa wito kwa watanzania kuacha mara moja maswala hayo na kurudisha
umoja na upendo miongozi mwa jamii.
Aidha katika hatua
nyingine kiongozi huyo ametoa pole kwa watanzania wote waliopatwa na janga la
Tetemeko mapema mwezi jana huku akitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwaombea
na kuwasaidia wahanga hao.
No comments