SERIKALI YARUHUSU WIMBO WA CHURA KUANZA KUPIGWA
Snura Mushi
Msemaji wa Msanii Snura Baraka Nyagenda. akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salamm leo.
Msanii
Snura Mushi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo, kuhusu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa
kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake,
Baraka Nyagenda.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa
kwa wimbo wa chura wa msanii Snura Mushi baada ya kuufunga kwa kuwa
haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Snura Mushi
alisema wimbo wake na video umeruhusiwa kupigwa baada ya audio ya chura
kufanyiwa marekebisho na kuifanya kuwa katika maudhui ya kitanzania.
Alisema
ruhusa hiyo imetolewa kwa barua iliyoaandikiwa Septemba 26, 2016 yenye
kumbukumbu HA.26/375/01’B’/137 ambayo gazeti hili lina nakala yake.
Kupitia
mkutano huo msanii Snura Mushi kwa mara nyingine aliomba radhi kwa
watanzania na Serikali kwa ujumla kwa usumbufu walioupata kwa video yake
ya kwanza na kuwaomba waendelee kuiona video mpya iliyorekebishwa baada
ya kuifuta ya kwanza.
No comments