IMPACTAFYA YAZINDUA KAMPENI YA KUKIMBIA / KUTEMBEA
KAMPUNI ya IMPACTAFYA imezindua rasmi
program ya Mazoezi Movement to Fitness kuhamasisha Watanzania kuwa na kaliba ya
kufanya mazoezi kuepukana na matatizo yatokanayo na kutofanya mazoezi.
Akizungumza na waandishi wa habari,
jana Habari Maelezo Mkurugenzi wa IMPACTAFYA, Bhakti Shah amewataka watanzania
kuamka na kulichukulia suala la kufanya mazoezi kuwa jambo la kupewa
kipaumbele.
Alisema Tanzania iko hatarini kupoteza
mamillioni ya watu ambao ni nguvu kazi ya jamii kwa kutofanya mazoezi, “Ugonjwa wa kisukari ambao kwa kawaida
huwapata watu wazima unaongezeka kwa haraka ulimwenguni pote na sasa hata
vijana wapo hatarini kwa sababu hawafanyi mazoezi, asilimia 20 hivi ya
vifo vyote vilivyotokea miongoni mwa watu walio na umri wa miaka 21 hadi
45, vilisababishwa na kukosa kufanya mazoezi.”
Alihoji kama Teknolojia Ni
Baraka au Laana? Bhakti alisema “Leo watu wana afya bora na wanaishi
muda mrefu zaidi kuliko wale walioishi karne nyingi zilizopita kutokana na mabadiliko
ya kiteknolojia ambayo imekuja na Vifaa vya kisasa vya matibabu, lakini ni
teknolojia hiyo hiyo iliyoleta mashine ambazo zimesaidia kupunguza kazi nyingi
ngumu na hivyo watu wengi waishi maisha ya kukaa tu bila kufanya mazoezi yakutosha.”
alisema
“Katika ripoti iliyochapishwa hivi
karibuni yenye kichwa cha habari International Cardiovascular Disease
Statistics, Shirika la Moyo la Marekani lilieleza kwamba “mabadiliko ya
kiuchumi, watu kuhamia mijini, usitawi wa viwanda, na kuenea kwa biashara za
kimataifa, na mitandao ya kijamii, imesababisha kuleta mabadiliko katika
mitindo ya maisha ambayo huchangia ugonjwa wa moyo.” Ripoti hiyo inataja “kutofanya mazoezi na kula vyakula
visivyofaa” kuwa mambo yanayochangia sana ugonjwa huo.
Alisema Mtindo wa maisha wa Leo wa
mijini, mfanyakazi anaweza kuketi mbele ya kompyuta karibu siku nzima, aende
mahali popote atakapo kwa gari lake, na atazame televisheni na kubrows kwenye
mitandao ya kijamii jioni yote, na hivyo kujiingiza katika maradhi ambayo
yamehatarisha maisha.
“Watu wengi zaidi wanapendelea
kutumia motokaa na pikipiki badala ya baiskeli, asilimia 25 ya safari zote
hazizidi kilometa moja hivi, asilimia 75 ya safari nyingi fupi hufanywa
kwa gari. Hii ni hatari” alisema.
Alisema, Teknolojia ya kisasa pia
imefanya watoto wakae tu bila kufanya mazoezi ya kutosha. Uchunguzi mmoja ulioonyesha
kwamba kadiri michezo ya video inavyozidi kuwa yenye kufurahisha na halisi,
ndivyo watoto wanavyotumia wakati mwingi zaidi kutazama televisheni na
vitumbuizo vingine ambavyo huwafanya watoto hao wakae tu bila kufanya mazoezi
ya kutosha.
Akiongela hatari za kukaa tu bila kufanya Mazoezi ya
kutosha alisema watu wengi
wanapatwa na matatizo ya kimwili, kiakili, na kihisia. Akitolea mfano, hivi
karibuni shirika moja la afya nchini Uingereza liliripoti kuwa “Watoto wasiofanya mazoezi wanaweza kukabili
hatari ya kutojiheshimu, kuwa na wasiwasi mwingi na mifadhaiko mingi.
Ripoti
hiyo ilisema kuna uwezekano mkubwa kwamba watoto hao watavuta sigara na kutumia
dawa za kulevya kuliko watoto wanaofanya mazoezi.
Bhaktti alieleza kuwa Watu wengi hupatwa
na shinikizo kubwa la damu, kiharusi na ugonjwa wa moyo, aina fulani za kansa,
ugonjwa wa mifupa, na uwezekano mkubwa wa kuwa wanene kupita kiasi kwa kula
vyakula vyenye kalori nyingi na kutofanya mazoezi.
“Swala la kutofanya mazoezi ni TIME BOOM . Matatizo na madhara yatokanayo na kutofanya
mazoezi ni ya Ulimwenguni Pote, ni wakati sasa Tanzania Kuamka. Tunayaita
mashirika, makampuni na watu binafsi kuungana nasi katika MOVEMENT TO FITNESS
kuliokoa taifa hili.
Alisema tayari zipo Nchi nyingi sasa
zinazoendesha kampeni zao za Kitaifa za kufanya mazoezi kama vile Mexico,
Brazili, Jamaika, New Zealand, Finland, Shirikisho la Urusi, Morocco, Vietnam,
Afrika Kusini, na Slovenia. inafaa kwa Tanzania kuwa na wasiwasi kuhusu hali ilivyo
sasa.
“Ingawa hatari za kutofanya mazoezi kabisa zimezungumziwa
sana, sisi tunasema si lazima uwe na membership card ya gharama kubwa kuwa na
afya bora. Unaweza kutembe na kukumbia na ratiba nzuri ya kufanya mazoezi hayo”
alisema.
“Kuendesha kampeni yetu tumewateua
machampion wetu “Shamim Mwasha, mmiliki wa blog ya jamii 8020fashions na Monica
Joseph, Mon Finance pamoja na wengine akiwemo msanii Manyolee ambaye ametunga
na kuimba wimbo wakwanza Tanzania kuhamashisha ufanyaji wa mazoezi.”
“Kupitia Movement to fitness tuna
kipengele cha Fun run walk ambayo yakwanza ilifanyika mwezi uliopita wa
september, fun run walk nyingine inafuata mwezi huu wa kumi, tarehe 8 siku ya
jumaamosi pale Golden tulip oysterbay kuanzia saa 10 hadi saa 1 usiku, ambapo
tutatoa mbinu mbalimbali za kuwa fit kiakili na kimwili. Tunawakaribisha
kujiunga nasi kwa kujiandikisha kupitia no ya simu 0754 694643 au email move@impactafya.com
“Kila mmoja wetu ana daraka la
kutunza afya yake mwenyewe. Jiulize, ‘je nimefanya mazoezi ya kutosha? Ikiwa
sivyo, ninaweza kufanya nini ili niongeze mazoezi yangu?’ unaweza kuwasiliana nasi na kujiunga na Movement
to Fitness ambayo inasimamia na kufuatilia mwendo wako mzima wa kuishi kama
mwanamazoezi.
________
Bhati Shah
Managing Director – IMPACTAFYA
No comments