SERIKALI YAKIRI UHABA WA DAWA HOSPITALINI
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amekiri kuwapo uhaba wa dawa na vifaa tiba katika hospitali za Serikali nchini.
Amesema uhaba huo wa dawa ni changamoto ya muda mfupi na Serikali inatafuta ufumbuzi wa haraka kuwahudumia wananchi.
Alikuwa
akizungumza Dar es Salaam jana wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi
wa wodi ya kina mama na watoto katika hospitali zote za rufaa za Mkoa
wa Dar es Salaam.
Samia
alisema anatambua changamoto zinazoikabili Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwamba ni ukosefu wa dawa.
“Natambua
katika hospitali zetu za rufaa tuna changamoto ya vifaa tiba na dawa,
lakini Serikali tunaifanyia kazi kila mwananchi aweze kupata huduma
hizo kama ilivyopangwa,”alisema.
Alisema
idadi watu wanaoongezeka katika Mkoa wa Dar es Salaam husababisha
msongamano wa wajawazito na watoto katika hospitali za Serikali na
kuwafanya kina mama walale chini au walale mbali na watoto wao.
“Kwa
mujibu wa takwimu za hivi karibuni, takriban wanawake 432 kati ya
vizazi hai 100,000, hufa kila mwaka kutokana na uzazi na asilimia 80 ya
vifo hivyo husababishwa na ukosefu wa vifaa tiba, umbali wa vituo vya
afya, upasuaji wa huduma za dharura ya upasuaji kwa wajawazito na
kuongezewa damu.
“Kwa
Mkoa wa Dar es Salaam peke yake, kuna zaidi ya hospitali 42 zinazotoa
huduma za dharura za uzazi kwa kasi ya ukuaji wa jiji na bado Serikali
inahitaji zaidi ya hospitali 30 ndani ya miaka 10 ijayo,” alisema.
Kwa
mujibu wa Samia, mradi wa ujenzi huo utagharimu Sh bilioni 4.5 kwa
hospitali tatu na kila hospitali yenye ghorofa tatu na uwezo wa kuwekwa
vitanda 150, itagharimu Sh bilioni 1.2.
Alisema
Serikali imejipanga kuhakikisha hospitali zote za rufaa zinaendelea
kuimarishwa ili kutoa huduma bora za afya ikiwamo afya ya mama na mtoto.
No comments