MAALIM SEIF AZIANDIKIA BARUA BENKI ZOTE NCHINI KUPINGA PROFESA LIPUMBA KURUHUSIWA KUFUNGUA AKAUNTI YA RUZUKU KWA JINA LA CUF
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amemdhibiti
mwenyekiti anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa
Ibrahim Lipumba kwa kuandika barua kwa benki zote ili kudhibiti ruzuku
ya chama isipite kwenye mikono ya kiongozi huyo.
Hatua
hiyo imekuja siku chache baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa,
kumtambulisha Prof. Lipumba Benki ya NMB Tawi la Ilala akitaka apewe
ushirikiano wa kufungua akaunti mpya ya chama.
Taarifa
kutoka ndani ya CUF zinasema kuwa juzi Maalim Seif, aliandika barua kwa
benki zote kuzuia hatua hiyo kwa kuweka zuio la mtu yeyote kufungua
akaunti ya chama.
“Unajua
hii vita si ya kitoto ni mapambano yaliyopo ndani ya CUF lakini yana
nguvu kubwa kutoka katika kila pembe ya watu wanaochukia upinzani. Na
pia wapo hata viongozi wakubwa wa dola ambao kila siku wamekuwa
wakifanya kazi ya kuivuruga CUF.
“Walitegemea
lakini tangu jana (juzi) Katibu Mkuu ameziandikia barua benki zote
nchini kuzuia mpango wa Msajili kutaka kuchepusha ruzuku ya chama na
kwenda katika mikono ya Lipumba na sasa nakala yake imepelekwa kwa
Msajili wa Vyama,” alisema mtoa habari wetu.
Hatua
ya Profesa Lipumba kufungua akaunti inatokana na barua aliyopewa na
Msajili wa Vyama vya Siasa ya Oktoba 6, mwaka huu iliyosainiwa na Naibu
Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza kwenda kwa Meneja wa Benki NMB
Tawi la Ilala.
Katika
barua hiyo yenye kumbukumbu namba HA.322/362/14/104 inamtambulisha
Profesa Lipumba kutakiwa kufungua akaunti mpya ya The Civic United Front
(CUF).
Siri
ya Profesa Lipumba kutaka kufungua akaunti mpya yenye jina la Chama cha
Wananchi CUF inadaiwa kutolewa na watumishi wa benki wa tawi hilo.
Prof.
Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa
Vyama Vya Siasa, huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama.
Ofisi
ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kupitia Sisty Nyahoza ilinukuliwa na
vyombo mbalimbali vya habari ikikiri kumtambulisha Profesa Lipumba kwa
Benki ya NMB ili aweze kufungua akaunti hiyo, hata hivyo ikikana kujua
matumizi ya akaunti hiyo.
No comments