Breaking News

PICHA: MISS KANDA YA ZIWA 2016 ANYANG'ANYWA HADHARANI ZAWADI YA GARI ALIYOPEWA


Ozona Miss Lake Zone Eluminatha Dominick akizungumza na Wanahabari baada ya kukabidhiwa gari Jumamosi Septemba 10, 2016.Gari ambalo inaelezwa kuwa leo Ijumaa Septemba 30,2016 amenyang'anywa gari hilo mbele ya kadamnasi
******
Tumepokea taarifa za awali ambazo zinaeleza kwamba mshindi wa Ozona Miss Lake Zone 2016, kunyang'anywa zawadi ya gari alilopewa.

Siyo taarifa nzuri kwa sababu waandaaji wa shindano hilo walisema gari limenunuliwa kwa zaidi ya shilingi Milioni 10 huku nyepesi nyepesi zikidai kwamba gari hilo lilinunuliwa kwa shilingi Milioni sita na laki tano.

Gari likalipiwa pesa nusu na nyingine ikabaki deni. 
Sasa leo akiwa Jijini Mwanza, Miss huyo mwenye gari lake amesimamishwa na kuambiwa gari linadaiwa hivyo aliachie.

Hii siyo habari nzuri na ni zaidi ya aibu kwa Miss kusimamishwa barabarani mbele ya kadamnasi na kunyang'anywa gari. Lakini pia siyo habari njema kwa waandaaji ambao ni Flora Talents Promotion na mdhamini mkuu, kampuni ya vipodozi ya Ozona.Tutawaletea taarifa kamili hivi punde....

Jumamosi ya Septemba 10, 2016 , kulifanyika kinyang'anyiro kikali cha kumsaka mlimbwende wa Kanda ya Ziwa, (OZONA MISS LAKE ZONE 2016), ambapo Mlimbwende, Eluminatha Dominick (pichani) kutoka mkoani Geita ameibuka mshindi miongoni mwa walimbwende 17 (baada ya mmoja kujitoa) waliokuwa wakiwania taji hilo.


Ushindi wa mlimbwende huyo ulionekana kuwafurahisha mamia ya watu waliohudhuria kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye Viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza, likiwa nimeandaliwa na kampuni ya Flora Talent Promotions chini ya Mkurugenzi wake, Flora Lauwo na kudhaminiwa na makampuni mbalimbali ikiwemo mdhamini mkuu, kampuni ya vipodozi ya OZONA pamoja na 102.5 Lake Fm Mwanza.


Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Mhe.Jeseph Linzwa Kasheku Msukuma, alisema ni furaha kubwa mkoa wa Geita kunyakua taji la Ozona Miss Lake Zone 2016 na kwamba matarajio ni kujiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua taji la Miss Tanzania 2016 ikiwa ni sawa sawa na matarajio aliyoyaeleza mlimbwende wa Ozona Miss Lake Zone 2016.
Chanzo-BINAGI MEDIA GROUP

No comments