MFUMUKO WA BEI WASHUKA KWA ASILIMIA 4.5
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za
Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Ephraim Kwesigabo
Dar es salaam
MFUMUKO wa bei wa
umeshuka kwa asilimia 4.5 mwezi Septemba kutoka asilimia 4.9 ya mwezi
Agosti mwaka huu kutokana na kupungua kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma
kwa mwezi uliopita.
Hayo yamebainishwa na
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS), Bw. Ephraim Kwesigabo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es salaam.
Kwesigabo amesema
kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei kumetokana na kupungua kwa kasi ya upandajiwa
bei za bidhaa na huduma mbalimbali ikilinganishwa na Mwezi Agosti .
“Mfumuko wa bei mwezi
Septemba umeshuka ukilinganisha na mwezi Agosti kutoka asilimia 4.9 hadi kufika
asilimia 4.5 kutokana na kushuka kwa upandaji wa bei za bidhaa na huduma”.
Alisema Bw. Kwesigabo.
Aidha aliongeza kuwa
mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji Baridi vimepungua hadi kufika
asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 mwezi agosti mwaka huu.
Kwesigabo amesema
kuwa ushukaji huo wa bei za vyakula na vinywaji baridi umetokana na kupungua
kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi
kilichoisha kwa mwezi Septemba mwaka huu.
Mbali na hayo
Kwesigabo amesema kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania imefikia shilingi 97.4
katika kununua bidhaa na huduma kwa mezi septemba ikilingfanishwa na shilingi
96.83 mwezi Agosti.
Aidha Mkurugenzi
Kwesigabo amesema kuwa anawaomba wananchi kwa ujumla kuendelea kutoa
ushirikiano wa dhati kwa Ofisi za takwimu Za Mikoa wakati wa ukusanyaji wa
takwi,u mbalimbali kwa maendeleo ya nchi yetu.
No comments