Breaking News

BI MARRY KINABO: NGUVU YA SOKO YA ATHIRI MAUZO YA HISA ZA DSE.

Afisa mwandamizi wa masoko (DSE) Bi, Marry Kinabo akifafanua jambo wakati akiwasilisha taarifa za soko wiki hii kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jiji dar es salaam



Na Frank Wandiba
 Kuongezeka kwa mauzo katika kaunta ya kampuni ya sigara tanzania nchini (TCC) ndio  chanzo kikuu cha kupanda kwa mauzo katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) wiki hii.

Akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la hisa wiki mapema leo jijini dar es salaam  Afisa mwandamizi wa Soko hilo Bi Mary Kinabo alisema hali hiyo imechangia mauzo ya hisa kuongezeka kwa asilimia 65 kutoka shilingi bilioni 19.6 hadi kufikia shilingi bilioni 32.2 kwa wiki hii .

Alisema Takwimu  zinaonesha idadi ya hisa zilizouzwa na kunuliwa imepanda mara nne kutoka milioni 2.4 hadi kufikia hisa milioni 9 juma hili, wakati mtaji wa makampuni ya ndani nao umepanda kwa asilimia 0.35 kutoka trilioni 8.1 hadi trioni8.13 kufatia kushuka kwa bei katika kaunta ya TBL .

 Adha Bi Kinabo alisema ukubwa wa mtaji wasoko umeshuka kwa asilimia 0.41 kutoka Trilioni 21.576 hadi kufikia shilingi Trilioni 21.49 hali iliyochangiwa na kushuka kwa bei katika kaunta za NMG pamoja na kampuni ya ACA.

Kwa upande wa Sekta ya Viwanda wiki imepanda kwa pointi 26.16 baada ya hisa za TBL kupanda kwa asilimia 0.77 wakati sekta ya huduma za kibenki na fedha wiki hii ikushuka kwa point 0.52 baada ya bei kushuka kwenye kaunta ya DSE kwa asimilia 1.54.

Bi, kinabo pia amezitaja kampuni tatu ambazo zinaongoza wiki hii kwa hisa zake kuuzwa na kununuliwa ambapo CRDB bank inaongoza kwa asilimia 70, ikifatiwa na kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) asilimia 25, wakati kampuni ya bia Tanzania (TBL) ikiuza aslimia 3.


 

No comments