KUFATIA KUSAMBAA VIDEO WALIMU WAKIMWAZIBU MWANAFUNZI WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA KUVULIWA MADARAKA KWA MWL. MKUU WA SHULE YA KUTWA YA SEKONDARI MBEYA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo wakati wa mahojiano
maalum juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia tukio la
Walimu wa mazoezi katika Shule ya Sekondari ya kutwa Mbeya leo Jijini
Dar es Salaam.
Na: Frank Shija, MAELEZO.
MAMLAKA husika ya nidhamu kwa
walimu imeagizwa kumvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kutwa ya
Sekondari ya Mbeya, Mwl. Magreth Haule kufuatia kutotoa taarifa juu ya
tukio la kushambuliwa kwa mwanafunzi Kidato cha tatu Shule hiyo
Sebastian Chingulu.
Ikizungumza na mwandishi maalum
kutoka Idara ya Habari –MAELEZO, leo Jijini Dar es Salaam ambapo, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene amesema kuwa
tukio hilo ni la kweli lilitokea tarehe 28 Septemba, 2016 lakini Mwalimu
Mkuu huyo akutoa taarifa, hadi ziliposambaa kwenye mitandao ya kijamii.
“Ninaagiza mamlaka husika za
kinidhamu kumvua madaraka mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbeya Kutwa
Mwl. Magreth Haule avuliwe madaraka kutokana na kukaa kimya huku kukiwa
na tukio la unyama dhidi ya mwanafunzi”. Alisema Simbachawene.
Alisema kuwa kwa mujibu wa
taarifa za awali zilizopatikana tukio hilo lilitokea huku ikidaiwa
chanzo chake ni mwanafunzi Sebastian Chingulu kugomea adhabu aliyopewa
na mwalimu wake.
Aliongeza kuwa walimu waliohusika
na tukio hilo ni wa mazoezi kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam
na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo walishirikiana
kumshambulia mwanafunzi huyo.
SImbachawene aliwataja walimu hao
wa mazoezi kuwa ni pamoja na Frank Msigwa kutoka DUCE, ambaye ndiye
chanzo kikubwa kufuatia madai ya mwanafunzi huyo kugoma kufanya adhabu
aliyopewa na mwalimu huyo.
Wengine ni John Deo na Sante Gwamoka kutoka DUCE,mwingine ni Evans Sanga kutoka Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Awali akielezea hatua ambazo
tayari Serikali imekwisha zichukuwa, alisema kuwa ni pamoja na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya kuendelea na ufuatiliaji wa karibu
suala hilo ambapo mpaka sasa vyombo vya dola vinaendelea kuwahoji baadhi
ya walimu washule hiyo.
Hatua nyingine ni pamoja na
kuendelea kuwasaka wahusika wa tukio hilo kwa kuwa mara baada ya kufanya
shambulio hilo walitoweka kusikojulikana, hata hivyo halisisitiza kuwa
hakuna hatakaye kwepa katika hili.
Katika hatua nyingine
Simbachawene aamewaagiza Wakuu wa Shule za Serikali nchini kuzingatia
kanuni za utoaji wa adhabu kwa wanafunzi badala ya kufanya kazi kwa
mazoea.
No comments