BANDARI YA DAR YAWEKA HISTORIA KWA KUPOKEA MELI KUBWA KULIKO ZOTE ZILIZOWAHI KUTIA NANGA BANDARINI HAPO.
Bandari
ya Dar es Salaam imeandika historia mpya kwa kupokea meli kubwa kuliko zote
zilizowahi kutia nanga Bandarini ikiwa na urefu wa mita 261.
Na Frank Wandiba
Meli
hiyo inayoitwa MV Hammonia Grenada ambayo ina uwezo wa kubeba makasha 4,256
imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam ambapo imeshusha makasha 483 na
kupakia makasha 656 kabla ya kuelekea nchini Thailand
.
Mkurugenzi
Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kwamba ujio wa meli hiyo ni
ushahidi tosha kwamba bandari ina uwezo wa kupokea meli kubwa za aina hiyo
ambazo awali zilikuwa zikiishia bandari ya Mombasa tu.
Kakoko
amesema kwamba wapo waliokuwa wakifikiri kwamba bandari yetu sasa haifanyi kazi
lakini ukweli ni kwamba bandari yetu ipo sawa na inaendelea kupokea meli kama
kawaida.
Na
kuwathibitishia hilo, amesema kwamba hata Mhe. Rais John Pombe Magufuli wakati
alipokuja kufanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam kulikuwa na meli
nyingine saba zimetia nanga.
“Napenda
niwatoa hofu wateja wetu kwamba bandari yetu ina uwezo wa kuhudumia meli kubwa
bila shida yoyote na ujio wa meli hii umefungua milango ya meli nyingine kubwa
kuja katika bandari yetu,” alisema Kakoko.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bandari ya Dar es Salaam ina gati zenye uwezo wa
kuhudumia meli kubwa za namna hiyo ambazo ni pamoja na gati namba 8,9 na 10.
Naye
Rubani Mkuu wa Mamlaka, Capt. Abdullah Mwingamno ambaye ndiye aliyeengiza meli
hiyo amesema kwamba hii ndio meli kubwa kuliko zote ambazo zimewahi kuingia
katika bandari ya Dar es Salaam.
Mwingamno
amesema kwamba hapo mwanzo mlango wa bandari yetu ulitengenezwa kuweza
kuhudumia meli zenye urefu wa mita 234 tu lakini kutokana na mabadiliko ya
teknolojia na jinsi meli zenyewe zinavyojengwa imeweza kuingiza hata meli za
urefu mkubwa zaidi.
Pamoja
na suala la teknolojia, Capt Mwingamno amesema kwamba kwa sasa TPA ina
wataalamu wa kutosha ambao wamepata mafunzo sehemu mbalimbali Duniani ili
kuweza kuingiza meli kubwa za namna hiyo.
“Tumepeleka
kundi la kwanza la vijana wetu nchini Afrika Kusini kupata mafunzo ya jinsi ya
kuingiza meli kubwa katika bandari yenye lango kama la kwetu na kundi la pili
la vijana hawa tumelipeleka Copenhagen, Denmark,” amesema.
Amesema
kwamba kundi la tatu la vijana hao tulilipeleka Nantes nchini Ufaransa kupata
mafunzo kama hayo, kwahiyo napenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba tunao
wataalamu wa kutosha kuifanya kazi hii.
Hapo
awali, TPA ilishawahi kuingiza meli nyingine kubwa yenye urefu wa mita 250 na
baadae ikaingiza meli nyingine yeenye urefu wa mita 255.
Kwa
mujibu wa Capt. Mwingamno, meli zenye urefu wa mita 261 mara nyingi huishia
Bandari ya Mombasa kutokana na udogo wa lango letu lakini ujio wa meli hii
umefungua rasmi milango ya kibiashara.
“Ujio
wa meli hii umefungua rasmi njia kwa meli nyingine kubwa za aina hii ambazo
zilidhani zisingiweza kuingia katika bandari ya Dar es Saam na hivyo kufungua
rasmi ushindani na bandari nyingine,” amesema.
No comments