TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL 500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba
akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa
Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya
Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia
ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na
kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za
Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo
Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na azingira,January Makamba akiwa
kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kulia ni Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Kaimu
Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani Richard Muyungi.
TANZANIA
inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka 2030 ili
kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea
katika maeneo mbalimbali hapa nchi.Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa
kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia
kupunguza juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya
tabia nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa
ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa
Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi.
Aliitaja baadhi ya miradi ambayo
itatekelezwa ili kupunguza gesi joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni
katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya
Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.
“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati
tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka
hazitaweza kuchukuliwa athari za kimazingira zinaweza kuendelea
kujitokeza”alisema Waziri Makamba.
Ambapo alisema katika kushiriki
juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari
serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia
mabadiliko ya tabia nchi .
Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa
sasa imeshaanza kutekelezwa katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na
Halimashauri mbalimbali hapa nchini.
“Juhudi za serikali ni kuhimiza
matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme
yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa
ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza
Waziri Makamba.
Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa
Mazingira kutoka wizarani Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye
mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali
nchini.
Alisema ilikuweza kuwa na mipango
madhubuti katika utekelezaji mkakati wa taifa wa mawasilinao wa
mabadiliko ya tabia nchi kupitia wizara za kisekta.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
No comments