TECNO YAZINDUA SIMU MPYA YA COMON C9 JIJINI DAR.
Kampuni maarufu ulimwenguni ya utengenezaji simu
janja za mkononi (Smartphone) ya Tecno Mobile imezindua rasmi nchini Tanzania smartphone
mpya aina ya Comon C9yenye uwezo na sambamba na kufanya promosheni kubwa kwa wateja wake 100 kuweza kujishindia
simu mpya CAMON C9Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa promosheni hiyo meneja wa
mauzo wa TECNO Mobile Tanzania, Bw.Fred Kadinala amesema kua TECNO inawajali
watumiaji wa simu zake hivyo kuamua kuwapa zawadi kubwa na kuwaruhusu waagize
simu kwa bei ndogo ili wapate simu hiyo mapema Zaidi.
Amesema toleo hili la Comon 9 C9 litaleta mapinduzi ya simu za smartphone kwenye soko la simu nchini kutokana na kusheheni sifa mbalimbali ikiwemo kamera yenye uwezo mkubwa wa mega pixel 13 mbele (selfie) na nyuma ambayo ni ya kwanza kwenye soko nchini
Kwa upande wake meneja wa kampuni ya simu ya Vodacom bwana
Dominic Mukama amesema kampuni inatambua bidhaa bora hivyo kwa kushikiana na
tecno wateja anaotumia mtandao wa Vodacom watakao nunua simu ya Comon C9 wanachotakiwa
kufanya ni kutuma neno OIMEI ikifuatiwa na nafasi kasha namba za IMEI kwanda
namba 15300 moja kwa moja atajipatia GB za bure.
Pia katika
uzinduzi huo Zawadi mbalimbali zilitolewa kama Tv ya Flat screen inchi 42 yenye thamani ya million moja na
nusu, pamoja na kadi ya Carlcare VIP card yenye thamani ya shilingi laki 3, itakayomuwezesha
mteja kutengenezewa simu yake bure mwaka
mzima kwa tatizo lolote litakalotokea na pia kifurushi maalumu cha zawadi
kutoka kampuni ya Tecno.
Aidha katika uzinduzi huo kulikuwa pia na
michezo mbalimbali ambayo washiriki zaidi ya mia moja waliojishindia zawadi mbalimbali
ikiwemo rice-cooker, jagi la umeme, oven, na vifurushi vya zawadi kemkem tokea
kampuni ya Tecno Mobile Tanzania
Sifa nyingine ambazo zinapatikana ndani ya simu ya
CAMON C9 ina betri yenye nguvu kubwa, memory card ya ndani yenye ukubwa wa GB
16, RAM ya GB 1, prosesa yanye nguvu ya GHz 1.3 inayofikia hadi GB 12.
No comments