Breaking News

TAARIFA KUTOKA DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE PLC (DSE)

                                                                             

TAARIFA KWA UMMA:
ONGEZEKO LA KIWANGO CHA MTAJI NA
MGAWANYO WA HISA KUFUATIA MAUZO YA AWALI (IPO) YA
DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE PLC (DSE)
Soko la hisa la Dar es salaam (DSE) iliendesha mauzo ya awali (IPO) ya hisa zake kuanzia Jumatatu tarehe 16 Mei 2016 hadi Ijumaa tarehe 3 Juni 2016 kwa matarajio ya kukusanya mtaji wa TZS 7,500,000,000 kutokana na mauzo ya hisa 15,000,000 kwa bei ya TZS 500/= kwa hisa moja.
Kufuatia mauzo haya ya awali DSE imefanikiwa kukusanya mtaji wa TZS 35,768,796,000 na kupitiliza kiwango cha mtaji kilichopangwa kwa asilimia 377%.
Kufuatia kutangaza matokeo ya mauzo ya awali tarehe 16 Juni, ombi la kuongeza kiwango cha mtaji kutoka TZS 8,250,000,000 hadi TZS 10,125,000,000 lilipelekwa kwenye mamlaka ya masoko ya mitaji (CMSA) na kwa ugawaji wa hisa kwa taratibu zifwatazo:
   i)            Waombaji wa hisa za hadi thamani ya TZS 5 milioni (hisa 10,000) watapata hisa zote;
 ii)            Waombaji wa hisa za thamani ya zaidi ya TZS 5 milioni (zaidi ya hisa 10,000) watapata hisa sawa na mgawanyo unaoendanda na ukubwa wa maombi yani pro-rata na pia watarudishiwa baadhi ya fedha zao kulingana na kiwango cha ugawaji.
iii)            Wafanyakazi wa DSE watapata asilimia 3 ya hisa.
DSE ina furaha kuutangazia UMMA kuwa mamlaka ya masoko ya mitaji (CMSA) imeidhinisha ongezeko la kiwango cha mtaji hadi kufikia TZS 10,125,000,000.
Vilevile DSE ina furahi kuutangazia UMMA kuwa ombi la ugawaji wa hisa kwa taratibu tatu zilizotangulizwa hapo juu pia limeidhinishwa na CMSA.
Baada ya ugawaji wa hisa, uratibu wa hundi za malipo ya pesa za ziada za maombi ya hisa utakamilishwa tarehe 7 Julai 2016 na usajili wa akaunti za CSD utakamilishwa tarehe 11 Julai 2016.
Ratiba ya kujiorodhesha na kuanza mauzo katika soko la Hisa la Dar es Salaam itaendelea tarehe 12 Julai 2016 kulingana na muongozo wa ratiba ya IPO ya DSE.
Mauzo ya hisa na kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es Salaam inafuatia mahitaji ya kisasa ya masoko ya hisa na yamekusudiwa kuleta ubora na tija katika utendaji wa uongozi wa DSE na zaidi katika kuimarisha utekelezaji wa mikakati na utendaji wake.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali rejea nakala ya muhtasari wa kampuni ya DSE unaopatikana kwenye tovuti yetu http://www.dse.co.tz/  

                                                                    Imetolewa na;
                                                                    Menejimenti
                                                  Dar es Salaam Stock Exchange PLC

No comments