JUMUIYA SHIA WAMKABIDHI MADAWATI RAIS DK.SHEIN
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Mohamed
Raza Daramsi wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo akifuatana na
Viongozi na Mashekhe wa jumuiya hiyo kwa ajili ya kukabidhi msaada wa
madawati 100 kwa ushirikiano na familia ya Rais wa Jumuiya,msaada huo
utaowanufaisha wanafunzi wa Skuli mbali mbali za Zanzibar
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akitoa shukurani kwa
Uongozi wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir wakati ulipofika Ikulu
Mjini Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia)
ikiwa ni katika kuimarisha sekta ya Elimu hapa Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mashekhe wa Jumuiya
ya Khoja Shia Ithna-asheir (kulia) Sheikh Shaaban Hussein,Sheikh
Maulana Dhishan Haidar na Rais wa Jumuiya hiyo Mhe, Mohamed Raza
(kushoto) wakati walipofika ikulu Mjini Zanzibar kukabidhi msaada wa
madawati 100 kawanafunzi wa Zanzibar,
Rais
wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-asheir Mhe,Raza (kushoto) akitoa maelezo
kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali
Mohamed Shein (kulia aliyekaa) wakati Jumuiya hiyo ilipofika Ikulu Mjini
Zanzibar leo kukabidhi madawati 100 kwa ajili ya wanafunzi wa Zanzibar
ikiwa ni katika katua za kuimarisha sekta ya Elimu nchini.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia)akikabidhiwa madawati 100 kutoka kwa Viongozi wa jumuiya
ya Khoja Shia Ithna-asheir na familia ya Rais wa Jumuiya hiyo Mohamed
Raza walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,msaada huo kwa ajili ya
wanafunzi wa Zanzibar,
No comments