IDARA YA URATIBU WA MAAFA YAKUTANA NA WADAU WA MASUALA YA MAAFA KUTOKA UMOJA WA KIMATAIFA.
Mkurugenzi
Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen, Mbazi Msuya
akizungumza jambo wakati wa kikao na wadau wa masuala ya Menejimenti ya
maafa kutoka Umoja wa Mataifa (UN) katika ofisi yake tarehe 05 Julai,
2016.
Mhandisi
wa Idara ya Uratibu wa Maafa Bw.Fanuel Kalugendo akizungumza jambo
wakati wa kikao cha kujadili masuala ya upunguzaji athari za maafa na
wadau kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa katika Julai 5, 2016 Jijini Dar
es Salaam.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa
kushoto) akiteta jambo na wadau wa masuala ya Menejimenti ya Maafa
kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Katikati ni Mwakilishi mkazi Umoja wa
Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez na Mratibu Bi. Mona Folkesson Julai 5,
2016.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua
(watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
wa Idara ya Uratibu wa Maafa na wadau wa masuala ya Maafa kutoka Ofisi
za Umoja wa Mataifa mara baada ya kujadili masuala ya menejimenti ya
Maafa Ofisini hapo Juali5, 2016.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments