Breaking News

SAGCOT WASAINI MKATABA NA MAKAMPUNI YALIYOOMBA UFADHILI KWA AJILI YA UKUZAJI KILIMO NA VIWANDA


01 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na vongozi wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, wawakilishi wa vyama vya wakulima na wawakilishi wa wabia wa Maendeleo jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko.

1 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo (Mwenye tai nyekundu waliosimama) akishuhudia  wawakilishi wa vyama vya wakulima wakisaini mikataba ya makubaliano ya ufadhili wa Fedha katika mfuko wa Kichocheo wa SAGCOT pamoja na kampuni zilizoibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha kuomba ufadhili kutoka kwenye mfuko huo jijini Dar es Salaam leo. wanaosaini hati hizo kutoka kulia ni Mkulima wa miwa Dk George Mlingwa Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Germao Cane Estate, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe, Roy Omulo kutoka kiwanda cha Maziwa cha Asas Dairies Iringa  na Lutengano Peter Mwenyekiti wa MUWAMARU Tukuyu mkoani Mbeya.


02 
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo amesema kuwa Mfuko wa SAGCOT wamesaini mikataba kwaajili ya kibiashara kwanzia mtaji kati ya Dola Za Kimarekani milioni 50 hadi 100 zitakuwa zikitolewa  kwa miradi kupitia madirisha ya Matching Grant Fund(MGF) ambao utakuwa ukitatua changamoto za wakulima na masoko yao.

2

Baadhi ya viongozi hao wakiwa katika mkutano huo leo

3

Baadhi ya wafadhili wakiwa katika mkutano huo

4

Washiriki wa mkutano huo kutoka makampuni mbalimbali na serikali

5 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joel Malongo akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko Kichocheo wa SAGCOT, Ami Mpungwe wakati wa mkutano huo.

No comments