Breaking News

PROF. LIPUMBA: CUF HATUNA MPANGO WA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHOCHOTE UCHAGUZI 2025

Chama Cha Wananchi (CUF) kimesema hakuna mpango wa kuungana na chama chochote cha siasa kuelekea uchaguzi mkuuq wabunge na rais 2025 kufatia kuwa ni moja ya waanga wa muungano wa vyama vya siasa mwaka 2015 kupitia UKAWA kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi.

Akizungumza makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam kuhusu msimamo wa chama kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema rejea kilichotokea uchaguzi wa mwaka 2015 kufatia kuunganisha vyama kwa dhati, kumbe chama kingine kipo kimkakati kudhoofisha vingine kutokana na uchu wa madaraka.

“Wakati tunaingia UKAWA, nikiamini tuko pamoja wakati na narudisha fomu ya kugombea kiongozi mmoja wa chama ambaye tulikuwa naye katika muungano huo alikuja kuniwekea pingamizi dakika za mwisho jambo ambalo liliniumiza sana,” alisema Prof. Lipumba

Alisema mda wa kujaza wa fomu kwa wagombea wa CUF, viongozi wa chama kingine waliwashawishi wajaze kama wagombea wanaotoka katika vyama vyao hatua hiyo inadhihirisha kulikuwa na mpango wa kudhoofisha vyama vingine

Profesa lipumba aliongeza Kufatia changamoto zilizojitokeza wakati huo wa kuunganisha vyama kwa lengo la kuwa na nguvu ya pamoja ili kuiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa sasa tuko Ngangali na chama hakina mpango wa kuungana na chama chochote katika uchaguzi wa mwaka huu.

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika miezi michache ijayo Prof Lipumba amesisitiza kuwa kufatia mapungufu yaliojitokeza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwaka jana Uchaguzi Mkuu ujao yafanyike marekebisho ya Sheria na Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na upatikanaji wa Katiba Mpya hili uchaguzi huo uwe huru na haki.

Aidha Prof Lipumba amewaka wazi kuwa kamati ya chama inayoshughulikia uwandaaji wa Ilani ya Uchaguzi inaendelea na mchakato huo kwa kutumia akili Mnemba (AI) ili kupata mawazo mapana ya kusaidia kufikia malengo stahiki.

“Kamati inaandaa ilani ya uchaguzi kwa kutumia akili Mnemba (AI) imani yetu itatatua changamoto mbalimbali zilizopo na kupata ilani iliyobora, pia watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa uchaguzi ni gharama, hivyo watuunge mkono kwa lengo la kuleta mabadiliko,” amesema.  

No comments