ADO SHAIBU: ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA NCHINI VITOE HUDUMA UPIMAJI SARATANI
Dar es salaam - Chama Cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kuhakikisha kila Zahati na Vituo vya Afya nchini vinakuwa na huduma ya upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi na ya Matiti.
Akizungumza mapema leo Machi 6, 2025 na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaibu akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chama Magomeni jijini Dar es Salaam baada ufunguzi wa matukio kuelekea siku ya wanawake Duniani ambapo kulikuwa na Shughuli mbali mbali za kijamii ikiwemo uchangiaji wa damu na upimaji wa Saratani.
"Tunaitaka Serikali kuhakikisha kila kituo cha Afya na Zahanati Nchini zinakuwa na huduma ya upimaji wa Saratani ya Shingo ya Kizazi na Matiti, hivyo ni lazima Serikali ihakikishe kila kwenye Kituo cha Afya na Zahanati kunakuwa na vifaa vya upimaji ," amesema Shaibu.
Shaibu ameshangazwa kusikia kuwa hata wanaume wanapata Saratani ya Matiti ambapo kwa asilimia 99 Wanawake ndiyo wanaopata Saratani hiyo huku Wanaume wakiwa ni asilimia Moja pekee.
Hivyo Shaibu ametumia nafasi hiyo kuwa wa mfano Wanaume kwa kupima Saratani ya Matiti lengo likiwa ni kuhamasisha na Wanaume kupima Saratani hiyo badaya ya kuwahamasisha Wanawake pekee.
Awali Shaibu baada ya kuzungumza na Ngome ya Wanawake wa Chama hicho, alitembela wajasiriamali uona bidhaa zao ambapo alibaini changamoto wanazokabiliana ikiwemo changamoto ya mitaji na Masoko ya bidhaa zao pamoja na urasimu uliopo katika upatikanaji wa Mikopo ya Halmashauri.
Kwamba wanaopata Mikopo Kwa urahisi ni wale wa vikundi vya watu wenye mahudiano na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa ACT Wazalendo Janeth Rite amesema kuelekea Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025 wameanza Kwa staili ya kipekee.
Kwamba wameanza kwa utoaji wa huduma ya kijamii ikiwemo upimaji wa Saratani ya Shingo ya Mlango wa Kizazi na ya Matiti, uchangiaji Damu pamoja na maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali.
No comments