MKUTANO WA TATU WA KAHAWA KUFANYIKA FEBRUARI 21 HADI 22 JIJINI DAR
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa taarifa kwa wakazi wa jiji la dar es salaam na maeneo ya jirani juu ya kuanza kwa mkutano mkubwa wa Kahawa wa nchi za Africa, February 21 na 22 na utakaozileta pamoja zaidi ya nchi 25.
Akizjngumza wakati akikagua maadalizi ya kuelekea mkutano huo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimatafa wa Julius Nyerere (JNCC) amesema mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya tatu nchini fursa kubwa kwa wafanyabiashara wajitokeze kwa wingi wahitumie kutumia fursa hii ambayo Rais Dkt. Samia ameileta katika Taifa letu.
Aidha, Mhe. Chalamila amesema kufatia mkutano huo baadhi ya barabara zinazoingia katikati ya jiji zitafungwa katika kipindi chote cha mkutano huo.
"Hututafunga barabara zote isipokuwa Barabara inayotoka Airport kuja mjini ile ya mwendokasi haitaruhusiwa mtu yoyote kupita bali zitatumika na wageni watakao kuwa wakiwasili kuja kushiriki katika mkutano huo",. Alisema Mhe. Chalamila.
No comments