HATUNA MPANGO WA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHOCHOTE UCHAGUZI MKUU 2025 - NCCR MAGEUZI
Dar es salaam - Chama cha NCCR Mageuzi kimesema kuwa akina mpango kwa sasa wa kushirikiana na chama chochote cha siasa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa wabunge na Urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa, bwana Haji Ambar Khamis amesema kutokana na rekodi zilizopo rejea uchaguzi wa 2015 umoja na ushirikiano na vyama vingine hauna tija isipokuwa ni kuishia kupata maumivu tu.
“Rejea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 Sisi kama chama tulipitia wakati mgumu sana tulikuwa na wagombea wanne wa nafasi ya ubunge nchi nzima aliyepata ni nafasi moja tu ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia hivyo kukosa nguvu na fedha kupitia umoja huo”. Alisema Bw. Khamis
Alisema Chama katika uchaguzi huo chini ya umoja wa vyama vya upinzani (UKAWA) tulikubaliana kugawana majimbo kutokana na ushiwishi wa mgombea wa kila chama katika baadhi ya maeneo lakini cha kushangaza CHADEMA na CUF waliamua kuweka wawakilishi katika majimbo hayo kinyume na makubaliano.
Bw. Khamis aliongeza kuwa kufatia kadhia hiyo chama hicho akitakuwa tayali tena na kusisitiza kusimamisha wagombea katika nafasi zote Rais, wabunge na madiwani.
Akizungumzia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lisu kama hakutakuwa na mabadiliko kutoshiriki Uchaguzi Mkuu ujao amesema chama hakitahusika na chochote na hatukubaliani na wala kutuungi mkono kauli na matamko wanayotoa. Mosi ni kutokana kutoshirikishwa, na pili ukifatilia kwa kina kauli hizo zinavinasaba vya kutaka kusababisha uvunjifu wa amani, chama akiwezi kuunga mkono kwani tunatambua na kuienzi Tunu ya Taifa ya amani aliyotuacha Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere.
"Kwa matamshi na matamko ambayo wamekuwa wakitoa mara kwa mara ukiachilia kutokushirikishwa kama chama atutaunga mkono na tutaendelea na mikakati yetu ya ndani ya chama kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu na tukigundua kuwa mpango huo unaweza kusababisha uvunjivu wa amani atutosita kukemea". Alisema Bw. Khamis
No comments