Breaking News

ALIYEKUWA MATIBU MKUU TLP RICHARD LYIMO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI TAIFA

Dar es salaam - Jumla ya wajumbe 84 wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama Cha Tanzania Labour Part (TLP) wamemchagua kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa na Katibu Mkuu amechaguliwa Yustas M.Rwamugira.

Akisoma hotuba katika ufunguzi wa Mkutano kabla ya uchaguzi umefanyika katika ukumbi wa Mrina Februari 2, 2025 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mwenyekiti wa Taifa (TLP) Hamadi Mkadam amesema mkutano kama huu ulifanyika miaka mitano iliyopita Legho Hoteli na alichaguliwa Augustino Mlema kuwa Mwenyekiti wa Taifa na kazi hiyo aliifanya kwa muda mchache kama miaka miwili ambapo aliaga Dunia(kufariki) tarehe 21/8/2022.


"Ni kawaida kwa mujibu wa katiba yeti chama chetu toleo la 2009 kukutana Kila baada ya miaka mitano ili kuchagua viongozi wa kusimamia chama miaka mitano mbele, kwa hiyo ninawashukuru kwa kuitika wito kuja hapa kwa ajili ya mkutano mkuu wa uchaguzi na mambo mengine ya kukijenga chama chetu",amesema

Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyaloza amesema kuwa mkutano huo ni halali aliyeitisha anatambulika kisheria na kikatiba.

Chama cha TLP kupitia kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika Oktoba 8,2024 Makao Makuu ya Chama hicho Jijini Dar es Salaam kimewafukuza wanachama 21 kuwa wanachama wa Chama hicho .

Akisoma wanachama waliofukuzwa Katibu Mkuu wa Chama Taifa Richard Lyimo amesema waliofukuzwa ni Dominata Rwechungura(Dsm), Ivan Maganza (Dodoma), Mariama Kassim (Dsm), Riziki Mganga (Dsm) Stanley Ndamugoba (Dsm), Mary Mwaipopo (Pwani),
Mohamed Mwinyi (Pwani), Ramadhani Gaugau (Morogoro), Laurian Kazimiri (Morogoro)

Wengine waliofukuzwa ni Nataria Shirima (Morogoro), Kinanzaro Mwanga (Arusha),
Godfrey Stivin(Arusha) ,Rashidpp Amir (Tanga), Twaha Hassan (Tanga), Tunu R.Kizigo (Tanga), Damari Richard (Dodoma), Hamadp H.Alawi (Pemba), Mohamed S.Hemed (Pemba), Mariam O.Hamis (Pemba)Mussa A.Fundi (Tabora), Mwajuma Mussa (Mwanza) Oswald Nyoni (Ruvuma)

Baada ya kufanya uchaguzi katika Mkutano wa leo Februari 2,2025 wajumbe wamemchagua Richard Lyimo kuwa Mwenyekiti wa Chama Taifa huku Johari Rashidi Hamisi akishika nafasi ya Makamu mwenyekiti kwa kupigiwa kura na wajumbe waliohudhuria mkutano huo.

Kwa upande wa Zanzibar nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeshikwa na Hamadi Mkadam kwa kupata kura 81,huku Mgao Kombo akipata kura 2 na kura 4 zikiwa zimeharibika.

No comments