Breaking News

RC CHALAMILA AZINDUA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA RAIS DKT. SAMIA HOSPTALI YA RUFAA YA MKOA YA TEMEKE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amezindua rasmi kambi ya matibabu ya Madaktari Bingwa na Bobezi wa rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayofanyika katika Hosptali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke kuanzia tarehe 13/01/2025 hadi tarehe 17/01/2025

RC Chalamila amewasihi wananchi wa Dar es salaam na maeneo ya karibu kuhakikisha wanatumia fursa hii muhimu ya kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa na bobezi walioletwa na Mhe Rais ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali kiafya kupata matibabu kwa gharama nafuu

Pia Mkuu wa Mkoa Mhe. Albert John Chalamila amewaasa wananchi wa Dar es salaam kuepuka kuchanganya siasa katika tiba kwani kwa kufanya hivyo Hospitali zetu zitakwenda vizuri na wananchi watafurahia huduma

"Afya ndio mtaji namba Moja kwa Kila binadamu hivyo yatupasa kuchangia gharama kidogo ili huduma hizi za Afya zikiwemo madawa, vifaa tiba, na umeme ziendelee kuzingatiwa kuliko kukosekana kabisa", alisema Mhe. Albert John Chalamila Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi kuwatumia vizuri Madaktari Bingwa na Bobezi hao zaidi ya hamsini (50) ambao wanatoa huduma za Magonjwa ya ndani, macho, pua, masikio, koo, kinywa na meno, huduma za kibingwa za wanawake na uzazi, huduma za watoto, upasuaji, mifupa, Afya ya akili, ngozi, utengamao pamoja na huduma nyingine nyingi zitakazotolewa na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali mbalimbali za Tanzania

Aidha Mhe. Chalamila ameongeza kuwa huduma nyingine ni pamoja na huduma za vipimo mbalimbali ikiwemo CT Scan, 4D Ultrasound, X-ray, Uchunguzi wa Mfumo wa chakula na Vipimo vya maabara kulingana na uhitaji ambapo madaktari bingwa hao watakuwepo hadi tarehe 17/01/2025 katika Hosptali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke.

No comments