Breaking News

MANDONGA AMPA TANO RAIS DKT. SAMIA KWA KUAMASISHA MICHEZO

Bondia Karim Mandonga akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari Makunduchi Villa Hotel, Ungindoni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makunduchi Villa Hotel, Mohammed Haji akizungumza na waandishi wa habari Ungindoni, Kigamboni jijini Dar es salaam
Bondia Karim Mandonga akionyesha mkanda alioshinda wa PST kwa waandishi wa habari Makunduchi Villa Hotel, Ungindoni, Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Dar es salaam - Bondia maarufu nchini, Karim Mandonga amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono mchezo wa ngumi ambapo amekuwa akitoa zawadi kwa washindi wa mapambano mbalimbali.

Akizungumza Makunduchi Villa Hotel, Ungindoni, Kigamboni jijini Dar es Salaam amesema lengo la kumshukuru Rais Dkt. Samia kutokana na jitigada zeke za kusapoti michezo nchini hususani mchezo wa ngumi ambapo yeye ni miongoni mwa mabondia ambao tayari wameguswa na zawadi yake.

"Hakuna mwingine kama Mama "Rasi Samia", nimekuja kumshukuru kwa namna anavyotusapoti Mabondia, tumeaona amekuwa akisapoti mchezo wa mpira wa miguu, kuwamekuwa na goli la Mama, sasa ni zamu yetu na sisi wa mchezo wa ngumi kupata zawadi yake," alisema Mandonga.

Mandonga alisema kuwa "sapoti" hiyo ya Rais Dkt. Samia inawapa hamasa mabondia wapambane na kushinda mapambano yao kwasababu watapata zawadi za mapromota pamoja na ya Rais Samia.

Hivyo Mandonga alieleza kwamba kwa makubwa anayofanya Rais Samia katika Sekta mbalimbali nchini ikiwemo hiyo ya michezo, Afya, elimu, miundombinu na nyingine, anafaa kuungwa mkono ili aendelee kufanya mazuri zaidi.

Aliahidi kujitolea kutangaza mazuri ya Rais Samia ili wananchi wayajue na hatimaye apewe mitano tena ya Uongozi katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.

Hata hivyo Mandonga alisema atampelekea zawadi ya mkanda wake wa PST alioupata katika pambano lake.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makunduchi Villa Hotel Mohammed Haji alisema amekuwa akimuunga mkono Mandonga kwa sababu amekuwa akiunga mkono mambo mablimbali yanayofanywa na Rais Samia.

Hivyo kwa sababu alikuwa na jambo la kuzungumza kuhusu Rais Samia akamsapoti kwa kumtengenezea mazingira ya kuzungumza na waandishi wa habari ili kufikisha ujumbe wake.

Hata hivyo Haji alitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono michezo ikiwemo mchezo huo wa ngumi.

Kuelekea mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika kwa uenyeji wa Tanzania, Kenya na Uganda Haji alitoa wito kwa wawekezaji kuwekeza kwenye ujenzi wa mahoteli kwani Kutakuwa na ugeni mkubwa. 

No comments