Breaking News

WADAU WA SEKTA YA FEDHA NCHINI WAADHIMIA KUJIKITA KUTOA ELIMU KUKABILIANA NA WATOA HUDUMA WASIO RASMI

Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja, akizungumza na wanahabari baada ya kutamatika kwa Jukwaa la Kwanza la Wadau wa Sekta ya Fedha 2024, lililofanyika kwa siku mbili tarehe 10 hadi 11 Desemba 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam - Wadau wa Jukwaa Fedha nchi wakubaliana kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa umma ili wananchi waweze kujua fursa zinazopatikana katika sekta hiyo pamoja na kuwabaini watoa huduma wasio rasmi.

Akizungumza wakati akifunga mkutano huo Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Dkt. Charles Mwamwaja amesema wadau kwa kauoi moja wamekubaliana kitilia mkazo swala la kutoa elimu kwa umma ili wananchi waweze kujua huduma mbalimbali zinavyotolewa na namna ambavyo wanaweza kufaidika na huduma hizo.
"Wadau kwa pamoja tumekubaliana kuwekeza nguvu zaidi katika kutoa elimu kwa umma itakayo wawezesha kutambua fursa zilizopo katika sekta hiyo na namna ya kuzitumia fusra hizo hasa upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya shughuli za maendeleo pamoja na kitambua watoa huduma za fedha wasio rasmi nchini". Alisema Dkt. Mwamwaja.

Aidha Dkt. Mwamwaja, amesema kupitia jukwaa hilo wadau wamekubaliana kwa kufanya hivyo wananchi wanaweza kufaidika na fursa zinazopatikana katika sekta hiyo hususani upatikanaji wa mitaji na kuweza kuweza kukabiliana na watoa huduma za fedha wasio rasmi.
Awali Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Huduma za Tehama, Dkt. John Sausi, akuzungumza wakati akiongoza mjadala kuhusu fursa za Huduma za Kifedha za Kidijitali katika taasisi za kifedha kama benki, taasisi ndogo za kifedha (MFIs), vyama vya ushirika vya akiba na mikopo (SACCOSS), na vikundi vya kijamii vya kifedha (CMGs) amesema jamii bado inahutaji kupatiwa elimu zaidi ili iweze kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana katika sekta hiyo.

Alisema pamoja na fursa nyingi zinazopatikana katika sekta hiyo jamii bado inatakiwa kupewa elimu zaidi ili iweze kuzifikia fursa mbalimbali hususani mikopo na mitaji hili kuweza kujiletea maendeleo.

Jukwaa hilo lililoanza tarehe 10 Desemba 2024 kwa kuzinduliwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), linawahusisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Fedha kutoka Sekta za Umma na Binafsi wakiwemo kutoka benki na taasisi za fedha, kampuni za bima, vyama mwavuli vya sekta ya fedha, vyama vya ushirika wa akiba na mikopo, vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha.

No comments