TCCIA NA DUBAI INTERNATIONAL CHAMBER WAINGIA MAKUBALIANO KUKUZA USHIRIKIANO WA KIBIASHARA
Dar es Salaam - Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Dubai International chamber wamesaini Makubaliano (MoU) yenye lengo la Kuimarisha sekta ya Biashara na Uwekezaji wa Pande Mbili
Kupitia makubaliano hayo, pande zote mbili zitaimarisha ushirikiano kati ya makampuni ya Dubai na Tanzania kwa kuandaa misheni za kibiashara, mikutano, matukio ya kibiashara. Kuadilishana uzoefu, pamoja na kubadilishana taarifa na kuhusu fursa za uwekezaji na ushirikiano wa kibiashara zilizopo baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano hayo Waziri wa Viwanda na biashara, Dokta Seleman Jafo amesema uhusiano kati ya Tanzania na Dubai hususani katika sekta ya Kibiashara ni wa miaka mingi na umekuwa ukikuwa siku baada ya siku na kupelekwa mahusiano komavu Kibiashara kati ya mataifa yetu.
"Makubaliano haya yamekuja wakatu muhimu ambapo Tanzania inaelekea kuwa wenyeji wa michuano mikubwa barani Afrika tumeshauriana na wawekezaji hao kuona kama wanaweza kuwekeza katika sekta ya mahoteli kuelekea michuano hiyo na tunatamani Yale mambo tunayaona kule Dubai na Abu Dhabi tuyaone na hapa". Alisema Dkt. Jafo.
Alisema serikali imeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji na wafanyabiashara tayari imeshaongea na wawekezaji wa nchini Dubai kuangalia namna watawekeza pia katika sekta nyingine ikiwemo madini na miuondombinu.
Kwa upande wake, Rais wa Chemba ya biashara Viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA), bwana Vincent Bruno Minja amesema makubaliano haya ya kihistoria kati ya Dubai na Tanzania huku ukizingatia Taifa hilo kwa miaka momgi limekuwa kama lango la kimkakati kwa bidhaa za Kitanzania kufikia masoko ya dunia.
Alibainisha kuwa kupitia makubaliano hayo TCCIA imejidhatiti kuwa jukwaa linalowezesha biashara kati ya Tanzania na Dubai, likihamasisha ukuaji wa kiuchumi kupitia ushirikiano wa kimkakati na kuongeza kuwa Makubaliano hayo Sasa yataonyesha mwanga baina ya Tanzania na umoja wa falme za kiarabu (UAE) kupitia Dubai.
Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chambers. Bwana Mohammad Ali Rashed Lootah amesema tunajivunia Makubaliano na TCCIA hii ni ishara njema ya ushirikiano Kibiashara ambao utaleta manuafaa kwa pande zote mbili.
Bw. Mohammad aliongeza kuwa thamani ya biashara isiyohusisha mafuta kati ya Tanzania na Dubai ilikua kwa asilimia 9% mwaka 2023, kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2.7 jambo ambalo ni ishara njema za ushirikiano.
Alisema Jumla ya makampuni 274 kutoka Tanzania yalisajiliwa kama wanachama hai wa Dubai Chamber of Commerce kufikia mwisho wa Septemba 2024 huku akiwashauri wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za Kibiashara nchini Dubai kwani Kuna mazingira bora na wezeshi ya biashara na uwekezaji
"Makubaliano haya ni ya kihiistoria ni moja ya fursa ya kipekee kujenga madaraja ya ushirikiano kati ya jumuiya za kibiashara za Dubai na Tanzania na kufungua njia mpya za ushirikiano wa kimkakati.". Alisema
No comments