Breaking News

VETA YASHIRIKI MAONESHO YA 9 YA SAYANSI NA UBUNIFU DAR ES SALAAM

Meneja Uhusiano kwa Umma Veta, Sitta Peter akizungumza katika Kongamano la Tisa la Maonesho ya Sayansi na Teknolojia linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam
Mvumbuzi wa kifaa cha kufundushia mfumo wa jua na muundo wa Atomu, bwana Ernest Maranya amwekezea mmoja ya washiriki wa maonyesho hayo alitembelea banda la VETA namna mfumo inavyofanya kazi katika Kongamano la Tisa la Maonesho ya Sayansi na Teknolojia linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
Mwalimu wa Chuo cha Veta Dar es salaam  bwana Alli Issa akifafanua jambo katika Kongamano la Tisa la Maonesho ya Sayansi na Teknolojia linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Dar es salaam - Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dar es Salaam kimejipamga kuendelea kutoa mafunzo kwa vitendo na ubunifu ili kusaidia kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hususani ugonjwa wa malaria na fangasi.

Kauli hiyo imetolewa mapema leo Novemba 2, 2024 na Meneja Uhusiano kwa Umma Veta, Sitta Peter mara baada ya ufunguzi wa maonyesho ya 9 ya sayansi na ubunifu yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam

Alisema katika kufanikisha hazma hiyo tayali chuo hicho kimefanikiwa kuibua bunifu 118 ambapo tayali bunifu 13 zimeingizwa sokoni na 45 zikiwa katika mchakato wa kuingizwa sokoni.

"Katika maonesho haya ya 9 tumekuja kuonyesha watanzania bunifu hizi muhimu ambazo tumeweza kufanikiwa kupitia mafunzo kwa wanafunzi nao kupitia elimu hiyo kubuni bidhaa hizo ambazo ni msaada katika mapambano dhidi ya Malaria, fangasi na UTI". Aliesema Bw. Sitta

Alisema chuo hicho kimejipanga zaidi kuhakikisha kinafanya tafiti na kubuni bidhaa ambazo zinaweza kuwa msaada kwa jamii kulingana na changamoto zinazowakabili

Naye Mvumbuzi wa kifaa cha kufundushia mfumo wa jua na muundo wa Atomu, Ernest Maranya amesema tayari kifaa hicho kimepata ruhusa ya kufundishia kwenye shule za msingi na sekondari baada ya kupata Ithibatia kutoka Wizara ya Elimu.

Pia Kutokana na hilo ametoa ombi kwa Serikali na wadau wa elimu kumsaidia mtaji ili aweze kutengeza kifaa hicho kwa wingi jambo litakalosaidia kufikia malengo ya kutawanywa kwenye shule mbalimbali nchini.

"Nimetumia muda mrefu Katika kubuni kifaa hiki na ninaamini wanafunzi wengi wataweza kuelewa vizuri somo la mifumo ya jua, hivyo naomba wa elimu wanisaidie mtaji ili niweze kutengeneza kifaa hiki kwa wingi," amesema." Malanya

Kwa upande wake, bwana Alli Issa ambaye ni mwalimu wa Chuo cha Veta Dar es salaam alisema chuo kubuni bidhaa mbalimbali na kuzipatia hati miliki ili kulinda bunifu hizo zisiweze kuchukuliwa au kuigwa na wengine na kwa bidhaa zote hata ambazo bado hazijaziingiza sokoni pia tunaendelea mchakato wa kupata miliki bunifu.

No comments