PROF. LIPUMBA ATAKA HAKI NA USAWA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025
Dar es salaam - Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi ( CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba ametoa wito kwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kuweka mazingira ya haki na usawa kuelekea uchaguzi mkuu ujao 2025 wa ili kuendelea kulinda na kukuza Demokrasia Nchini.
Akizungumza makao makuu ya chama hicho Disema 29, 2024 wakati akitoa tathmini ya mambo mbalimbali yaliyojili mwaka 2024 hususani uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uchaguzi wa ndani wa ngazi ya taifa wa chama hicho wa kuwapata viongozi wa ngazi ya kitaifa wa chama katika nafasi mbalimbali.
Akizungumzia uchaguzi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa iliofanyika mapema Novemba 27, 2024 amesmea wote mashahidi uchaguzi huo ambao uligubikwa na dosari nyingi tangu mchakato wa awali pia ulikuwa uhuru na haki hasa kwa wagombea wa vyama vya upinzani kutokana na Demokrasia kusiginwa na TAMISEMI iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi huo.
"Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vitongoji na Vijiji uliofanyika Novemba 27, 2024 kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kusambaa kwa karatasi bandia za kupigia kura, baadhi ya wagombea hasa wa vyama vya upinzani kuenguliwa, baadhi ya maeneo majina ya baadhi ya wanachi kutoonekana kwenye daftari la mpiga kura, itoshe kusema uchaguzi huo ahukuwa huru na haki". Alisema Prof. Lipumba.
Alisema pamoja na dosari zote hizo zilizojitokeza kabla na wakati wa zoezi la uchaguzi bado Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa Novemba 29,2024 alitangaza matokeo ambayo yaliwezesha kuipa ushindi CCM kwa zaidi ya asilimia 90.
Aidha Prof. Lipumba abainisha kuwa CUF aitokubali dosari zilizojitokza katika Serikali za Mitaa kutokea tena katika uchagzi ujao wa Madiwani, Wabunge na Rais utakaotarajiwa kufanyika 2025 huku akisisitiza umuhimu wa Rais Dkt. Samia kusisitiza uwepo wa uhuru na haki katika uchaguzi huo.
"Nitoe rai kwa Rais Samia kuhakikisha kuwa kunakuwepo mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi wa uhuru nawa haki 2025, kwani kwa haya yanayoendelea itafikia hatua wananchi uvumilivu utafikia kikomo hivyo tutalitumbukiza Taifa letu kwenye machafuko ". Alisema Prof. Lipumba na kuongeza kuwa
"CUF tunayo imani Rais Dkt. Samia ameteleza katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji uliofanyika mapema Novemba 27, 2024 hivyo tunamtaka kutafatakari kwa kina na kuchukua hatua ya kurekebisha mambo kuelekea uchaguzi ujao kwa kuiwezesha iwepo tume huru ya Taifa ya uchaguzi kutekeleze majukumu yake kwa uhuru na haki.
Akizungumzia sekta ya Elimu na Afya nchini Prof Lipumba ameishauri Serikali kuhakikisha inawekeza kwa tija katika sekta ya Elimu, Afya hasa katika Rasilimari watu ili kuhakikisha Taifa lina vizazi vyenye Elimu bora, Afya bora hivyo kuwa na Uchumi imara kwa maendeleo Taifa.
No comments