Breaking News

MATOKEO YA TAFITI YAPELEKWE KWENYE MAENEO YALIYOFANYIWA TAFITI HIZO’ DKT. DUGANGE


Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Dkt. Festo Dugange amesema Ili tafiti ziweze kuwa na manufaa lengwa ni lazima matokeo na mapendekezo ya tafiti hizi yawafikie walengwa hivyo ni utoaji wa matokeo ya tafiti yakatolewe kule tafiti zilipofanyika ili walengwa, wananchi, viongozi na watendaji watakaohusika na matumizi ya matokeo ya tafiti hizi wawepo. 

Ameongeza kuwa Changamoto kubwa inayokabili vyuo vyetu katika eneo la Tafiti ni matokeo ya tafiti nyingi kuishia kwenye machapisho ya kitaaluma na kubakia kwenye makabati ofisini na hazifikishwi kwa walengwa.

Mhe. Dkt. Dugange ameyasema hayo leo akimuwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati wa wa Mahafali ya 16 ya chuo hicho iliyofanyika Kampus kuu ya chup hicho iliyoko Hombolo jijini Dodoma.
Amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini bado zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na uhaba wa wataalamu, ukusanyaji mdogo wa mapato na usimamizi usioridhisha wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati kwa baadhi ya Halmashauri, pamoja na shughuli nyinginezo. 

Chuo cha Serikali za Mitaa kina nafasi na jukumu kubwa la kuisaidia Serikali katika kutatua changamoto hizo kupitia mafunzo, tafiti na ushauri wa kitaalamu. 

Bado mafunzo, tafiti na ushauri elekezi vina nafasi kubwa kusaidia katika kubaini namna ambavyo changamoto za Mamlaka za Serikali za Mitaa zitakavyoweza kutatuliwa kwa kutoa wataalamu waliopikika vizuri, kufanya tafiti zinazolenga kutoa majibu katika changamoto hizo, lakini pia kutoa mafunzo ya muda mfupi yenye kuleta mabadiliko chanya katika utendaji’ amesisitiza

Napongeza jitihada za Chuo hiki kuendelea kufadhili tafiti kila mwaka zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali katika Serikali za Mitaa lakini matokeo ya tafiti hizo yakatolewe kule kwa wananchi ambao walihisika kufanyiwa tafiti ili wafahami changamoto ya maeneo yao na kuona namna wanavyoweza kuzitatua’ amesema Dkt. Dugange.




 

No comments