KAMATI YA MASHINDANO YA KHIMJI SUPER CUP YAKUTANA NA VILABU SHIRIKI ILALA
Dar es salaam - Kamati ya mashindano ya ya Khimji Super cup 2024-2025 imekutana na vilabu 12 vitakavyoshiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa hii leo katika uwanja wa Garden ilala jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Viongozi shiriki wa vilabu hivyo Mwandaaji wa mashindano hayo na mjumbe wa chama cha soka wilayani ilala IDFA ambaye pia ni Diwani wa kata ya ilala Mhe.Saad Khimji(Hom Boy) amevitaka vilabu hivyo kuzingatia nidhamu na weledi katika mashindano hayo.
Khimji ameawashauri viongozi wa vilabu hivyo kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wachezaji wao katika kudumisha umoja Amani na Upendo katika michuano hiyo ili kuleta matokeo chanya na sifa njema kwa wilaya hiyo itakayowasaidia kufika mbali zaidi kisoka.
Amesema lengo la kuanzisha michuano hiyo ni kupeana heshima kuibua vipaji lakini kikubwa ni utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi katika sera yake ya kutambua sekta ya michezo na kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoiheshimisha michezo hapa nchini.
Aidha khimji ametumia fursa hiyo kuwataka wakazi wa ilala na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja hivyo vya Garden kuja kushuhudia michuano hiyo yenye hadhi na mvuto wa kipekee katika wilaya hiyo.
"Tunawaomba mashabiki na wapenzi wa soka kuja kwa wingi katika viwanja vya Garden hapa ilala kuja kushuhudia vipaji mbalimbali ndani ya wilaya yetu" amesema khimji.
Khimji amesema Michuano hiyo inatarajiwa kuzinduliwa hii leo kwa kuzikutanisha timu za Kasulu na Mtendeni katika viwanja hivyo vya Garden ilala ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa ilala na Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu pamoja na Viongozi wengine wa Soka,Vyama na serikali.
Mshindi wa kombe la michuano hiyo anatarajiwa kujinyakulia zawadi ya Tshs.laki 5, medali ya dhahabu jezi na Mpira.
No comments