Breaking News

DC KINONDONI TUJITOKEZE KWA WINGI KUSHUHUDIA HISTORIA IKIANDIKWA USIKU "KNOCK OUT YA MAMA

Dar es salaam - Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Saad Mtambule amepongeza kampuni ya mchezo wa ngumi hapa nchini Mafia Boxing Promotions kwa kuja na ubunifu wa kuandaa pambano maalum kwa ajili ya kuenzi Kazi zinazofanywa na Serikali litakalofanyika jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza kuelekea siku ya pambano hilo katika ofisi za Mafia boxing Promotions zilizopo Magomeni Usalama Jijini Dar Es Salaam Mhe. Mtambule amesema katika pambano hilo la kwanza la kihiistoria nchini mgeni rasmi anatarakiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasim Majaliwa.

Alisema katika siku za hivi karibuni mchezo wa ngumi umekuwa na hamasa kubwa kufatia kampuni ya Mafia boxing kujitosa na kuonyesha kwa vitendo kuunga mkono juhudi za Serikali Chini ya Rais Dkt Samia katika michezo.

"Siku ya desema 26 ni siku ya kihiistoria kutakuwa na mapambano yatayowakutanisha mabondia kutoka ndani na nje ya nchi ambapo mikanda mitano ya uzito mbalimbali ya kimataifa nitoe rai kwa wakati wa jiji la dar es salaam na maeneo ya jirani kuja kujionea jinsi mabondia hao watakavyozioata katika ukumbi wa Superdome masaki" Alisema Mhe. Mtambule.

Nae Mkurugenzi wa Mafia boxing Promotions, bwan Ally Zayumba akizungumzia juu ya maandalizia ya pambano hilo amesema kila kitu kipo sawa na ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali kupitia Mkuu wa wilaya kwa kuwapa ushirikiano na ushauri katika maandalizi yote kuelekea pambano la knock out ya mama sehemu ya pili.

Amesema lemgo kubwa la kuandaa pambano hilo litakalofanyika Siku ya boxing day Disemba 26, 2024 ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo hapa nchini.

Alisema siku hiyo zaidi ya wageni 40 kutoka nje ya nchi wakiwemo mabondia ambao wataanza kupokelewa kuanzia leo jumatatu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar Es Salaam.

"Katika pambano hilo jumla ya mikanda mitano ambayo ni WBO,IBA, WBA, BST itashindaniwa
Ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyika hapa nchini ambapo mabondia wa Tanzania watapanda ulingoni kuzichapa na mabondia kutoka nje ya nchi". Alisema Bw. Zayumba

Alisema nichukue nafasi hii kuwakaribisha wadau na wapenzi wa mchezo wa ngumi wote siku ya Christmas ambapo mabondia wote watapima uzito pale Coco beach kuanzia sa 4 asbuhi.

Kwa upande wake msemaji wa kampuni ya Mafia boxing Promotions ambaye pia ni mwigizaji Juma Mafufu alisema siku ya pambano hilo hakuna mkanda hata mmoja ambao utaachwa na mabondia wa Tanzania na baadaye mikanda hiyo itapelekwa Ikulu kutokana na mapambano hayo kuwa maalum kwa ajili ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Pambano la "KNOCK OUT YA MAMA" litafanyika Desema 26,2024 katika ukumbi SuperDome Masaki kuanzia saa 7 mchana.

No comments