BONDIA AFARIKI DUNIA BAADA KUPIGWA TKO TANDALE KWA MTOGOLE
Dar es salaam - Bondia Hassan Mgaya amefariki dunia baada ya kupigwa TKO katika pambano la raundi sita lililofanyika Tandale kwa mtogole.
Mgaya alicheza pambano hilo lililofanyika usiku wa jana tarehe 28 Desemba 2024 jijini Dar es Salaam ambalo halikua la ubingwa na kupigwa TKO katika raundi ya sita dhidi ya aliyekua mpinzani wake Paulo Elias.
Kwa mujibu wa taarifa niliyopewa na chanzo cha kuaminika kilichokuwepo kwenye eneo la tukio marehemu Mgaya alidondoka ulingoni baada ya mwamuzi kumaliza kumuhesabia ambapo pambano hilo liliisha kwa matokeo ya TKO.
"Mgaya alipigwa na kwenda chini mwamuzi akamuhesabia ikawa TKO, baadae marehemu aliamka akatembea hatua kadhaa hapohapo ulingoni kisha akaanguka na kuzimia"
"Baada ya tukio hilo marehemu akapewa huduma ya kwanza kutoka kwa madakatari waliokuwepo kwenye pambano alizinduka na kupelekwa hospital ya Sinza kwaajili ya matibabu," kilichesema chanzo hiko.
Mara baada ya marehemu kufikishwa hospital ya Sinza akapatiwa rufaa ya kupelekwa hospital ya Mwananyamala leo na ndipo umauti ulipomkuta.
Pambano hilo lilifanyika Tandale kwa mtogole jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Dunia ndogo na waandaaji wa pambano hilo ni Golden gloves wakishirikiana na Ngoswe uwezo.
Akizungumzia tukio hilo bondia Cosmas Cheka ambaye ni muweka hadhina wa chama cha mabondia nchini Tanzania amesema suala la msiba wa marehemu Mgaya wanalisimamia wao kama mabondia kuanzia mwanzo wa hadi mwisho wa mazishi.
Pia Cheka amesema wao kama chama cha mabondia nchini wapo mbioni kuandaa utaratibu kumsimamisha muandaaji wa pambano hilo Haji Ngoswe.
"Nimewasiliana na mwenyekiti wetu wa chama cha mabondia Tanzania, Japhet Kaseba kuandika barua ya kupeleka TPBRC ya kumsimamisha promota Haji Ngoswe kwa kutoonesha ushirikiano kwa bondia aliyefariki," amesema Cosmas Cheka.
Mazishi ya bondia Mgaya yatafanyika kesho Desemba 30, 2024 Kiwalani jijini Dar es Salaam.
No comments