VIONGOZI MLIOCHAGULIWA KATATUENI CHANGAMOTO KWENYE MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI VYENU
Dar es salaam - Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu CPA Amos Makalla akizungumza na Waandishi wa Habari amewataka Viongozi waliochaguliwa kwenda kuwafanyia kazi Wananchi kama walivyoomba na kuacha tabia za urasimu kwa Wananchi.
Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA. Amos Makalla kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Novemba 29, 2024 katika Ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini ,Dar es Salaam.
"Tunaomba hao walioweza kushinda pale watakapo anza majukumu yao ,wameomba utumishi na Chama cha Mapinduzi kitaendelea kuwasimamia kuhakikisha kwamba wanaenda kuwa watumishi na kwenda kufanya kazi lakini Chama kinawaelekeza wote waliochaguliwa wakatatue kero mbalimbali kwenye Mitaa , Vijiji na Vitongoji vyao huku wakiendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi."
"Katika Serikali za Mitaa tunataka Viongozi hawa wawajibike kwa Wananchi kwa kusoma taarifa za mapato na Matumizi katika maeneo yao pamoja kuondoa urasimu wa kutoa huduma pale Wananchi wanapohitaji".
No comments