Breaking News

SERIKALI NA KAMPUNI YA CECIS YA CHINA WASAINI MAKUBALINO KUWEKEZA SEKTA YA MAWASILIANO

Na Neema Mpaka
Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania yatiliana saini ya makubaliano ya uwekezaji na mafunzo na Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Kielekroniki ya China (CECIS LTD),

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Maryprisca Mahundi amesema Tanzania inakwenda kupiga hatua kubwa katika masuala ya uchumi wa kidijitali.

Naibu Waziri Mahundi akizungumza leo Oktoba 21, 2024, katika hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam

Amesema kupitia makubaliano hayo, zaidi ya makampuni 600 ya vifaa vya kompuya yataweza kuwekeza nchini.

Aidha amesema lengo la uwekezaji huo ni kuongeza ujuzi kwa vijana na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utengenezaji wa komputar kimataifa.

Kwamba makubaliano hayo ni matokeo ya ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini China aliyoifanya hivi karibuni, Kampuni hii ni wabobezi wa masuala ya usalama wa mitandao hivyo elimu waliyonayo itawawezesha vijana kujifunza kwani tunahitaji wataalam wengi zaidi wa TEHAMA nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Abdulla amesema uwekezaji huo utatoa fursa kwa Watanzania kujifunza na kupata ajira.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya huduma za mawasiliano ya kielekroniki ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia wa Kamati ya Kampuni hiyo, Guo Zhaoping amesema uwekezaji huo umefuata misingi ya nchi za Tanzania na China na kwamba unalenga kuchochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali.

“Kampuni yetu inafanya uwekezaji katika mambo makuu matano ikiwepo sekta ya kompuya na usalama wa mitandao ambapo pamoja na kufanya shughuli za kibiashara pia tunalenga kukuza uchumi wa kidijitali baina yetu na nchi zingine, kwa hapa Tanzania tutafanya kazi kulingana na mahitaji” amesema Zhaoping.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dk. Nkundwe Mwasaga amesema pamoja na mambo mengine, pia wamekubaliana kuvutia makampuni mbalimbali ya Kielekroniki kuwekeza nchini ambapo mwaka 2025 kutakuwa na maonesho makubwa ya utengenezaji wa vifaa vya kompuya Afrika ambapo Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Tume yake watakuwa wenyeji wa maonesho hayo.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mohammed Abdulla na Mwenyekiti wa Kampuni ya huduma za Mawasiliano ya Kielekroniki ya China (CECIS) Guo Zhaoping

No comments