Breaking News

MHE. SILAA AIASA POSTA KUONGEZA UFANISI NA UBORA WA HUDUMA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Jerry William Silaa (Mb) amelitaka Shirika la Posta Tanzania kuongeza ufanisi na ubunifu katika utendaji wake ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi zinazokidgi matarajio yao

Aidha, Mhe. Silaa ameitaka Posta kuboresha huduma zake kidijitali ili kuendana na mkakati wa Serikali wa Tanzania ya Kidijitali chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Waziri ametumia nafasi hiyo kulisisitiza Shirika la Posta kuchangamkia kila fursa mpya za usafirishaji wa bidhaa,mazao,vitu vya thamani na huku akiahidi kuendelea kushirikiana na Shirika katika kuendeleza mabadiliko ya Posta kidijitali
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Ya Posta Balozi Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi ameahidi, Uongozi wa Bodi uko tayari kusimamia mageuzi ya uendeshaji ndani ya Shirika ili kukidhi matarajio ya wateja wake.

Kwa upande wake Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo ameelezea mpango mkakati wenye vipaumbele vya Shirika vinavyolenga kufanya mageuzi ya Posta ya Kidijitali ili kukidhi mahitaji ya wateja hasa katika kipindi hiki cha maendeleo makubwa ya Teknolojia




No comments