Breaking News

ACT WAZALENDO YABAINI MAPUNGUFU ZOEZI UANDIKISHAJI WAPIGA KURA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Chama cha ACT Wazalendo kimebainisha mapungufu makubwa ikiwa ni siku moja kabla ya ufunguzi wa zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika nchi nzima Novemba 27, 2024.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama, Ado Shaibu amesema kasoro hizo si kwa bahati mbaya bali ni moja ya mkakati wa makusudi ulioratibiwa ili kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM) kupata viti vingi vya uwakilishi wa wananchi.

"TAMISEMI wametoa Kanuni na Mwongozo kuhusu mchakato mzima wa Uchaguzi lakini katika zoezi la Vyama vya Siasa kutoa Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura imeishia kuelezwa kuwa ni haki ya vyama kupeleka Mawakala katika vituo vya kuandikisha Wapiga Kura tu,". Alisema Shaibu 

Alisema chama tunafikiri, Kuma TAMISEMI kama ingekuwa na nia njema na Uchaguzi huu, walivyotoa ratiba ya matukio mengine ya kiuchaguzi, suala la Vyama kuweka mawakala pia lingekuwa katika Kalenda au kwenye hoja ya Ufafanuzi wa Waziri.

Ameyatajia mapungufu hayo kuwa ni:

Msosi: Hakuna mtiririko juu ya utoaji wa taarifa na maelekezo kuhusu utaratibu mzima wa Uchaguzi,kila ngazi na kila eneo, Wasimamizi au Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi huu na kwamba wanatoa taarifa wajuavyo wao na kwa muda wanaoupanga wao.

Pili: Katika baadhi ya maeneo Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wamewapelekea barua viongozi wao wa Chama kuwataka wapeleke Orodha ya Mawakala wa Kusimamia zoezi la Uandikishaji Wapika Kura.

Kwamba barua imepokelewa Oktoba7, 2024 mchana huku wakiambiwa mwisho wa kuwasilisha majini ya Mawakala ni Oktoba 8, saa kumi jioni, huku ikibainishwa kiwa siku ya kuapisha Mawakala ni Oktoba 9, 2024 ingawa barua hizo zinaonekana kuandikwa Oktoba 5, 2024. 

"Swali la kujiuliza kwa nini zimechelewa kupelekwa katika Vyama. Mfano wa maeneo hayo ni Arumeru Mashariki, Arusha Mjini," amehoji Shaibu.

Tatu: kuhusu maeneo ya kuwaapisha Mawakala, amesema kwa Mujibu wa Kanuni ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Kifungu cha 48 (1) (e), imewataja Mawakala kuwa ni miongoni mwa watu wanaopaswa kula kiapo mbele ya Hakimu.

Lakini Kifungu cha 48 (2) kimeeleza ikiwa Hakimu hawezi kupatikana, Wasimamizi au waismamizi wasaidizi wanaweza kuwapa viapo Mawakala katika maeneo yao.

Hivyo amebainisha, hali ilivyo sasa, Wasimamizi wasaidizi kwa makusudi kabisa mbali ya kuchelewa kuwapa taarifa viongozi wao kuhusu utaratibu wa kupeleka Mawakala, lakini bado wamewataka Vyama kupeleka Mawakala katika kituo kimoja ili kuapishwa kinachojumuisha wilaya nzima au zaidi ya jimbo moja ambapo hisia zao ni kuhakikisha vyama havifanikiwi kupeleka Mawakala kwa kuwa wengi watashindwa kumudu gharama za nauli na muda pia.

Ametoa mfano Wilaya ya Kinondoni ambapo Mawakala wa majimbo ya Kinondoni na Kawe wametakiwa kwenda kuapisha katika kituo cha shule ya Sekondari Turiani iliyopo karibu na ofisi ya Manispaa ya Kinondoni, huku vituo vya kuandikisha vikiwa 207.

Amesema Newala, Viongozi wao wa Chama wametakiwa kuwapeleka Mawakala wote Newala Mjini kwenda kuapishwa ambapo baadhi ya Maeneo yanazaidi ya Kilometa 70 mfano yale yanayopakana na Msumbiji.

Kwa Bagamoyo, katika Kata ya Yombo ametoa mfano kuwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi amewaita viongozi wa vyama ambapo ametoa taarifa ya kikao tarehe 9 asubuhi na kikao ni tarehe 9 saa tano kwamba vyama vipeleke Mawakala tarehe 9 Mchana ili tarehe 10 waweze kuapishwa.

Kwamba baadhi ya maeneo, Viongozi wao wametakiwa kupeleka majina ya Mawakala wakiambatanisha na nakala ya Picha za Pasipoti kwa kila wakala ili kuwatambua, kinyume kabisa na miongozo na Kanuni ya Uchaguzi ambapo ametolea mfano Kibiti eneo la delta.

Nne: Upangaji wa Vituo, amesema Mwongozo kuhusu Upangaji wa vituo vya Uandikishaji wapiga kura umeonesha Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kwa kushirikiana na Vyama vya siasa watapanga na kukubaliana mahala patakapotumika kwa zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura na kutoa kipaumbele katika maeneo ya Umma au pale patakapokubaliwa. 

"Yapo maeneo mengi Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wamejipangia maeneo ya kuandikisha Wapiga Kura bila kuvishirikisha vyama na hasa vya Upinzani Mfano Tanga Mjini ambapo viongozi wetu wanaona kuwa maeneo mengi yaliyoteuliwa yameangaliwa kimkakati kwa ajili ya kutoa fursa kwa CCM," amesema.

Tano: siku ya Uchukuaji wa Fomu, kwamba kwa Mujibu waKanuni ya Uchaguzi na Kalenda ya Matukio, TAMISEMI wameonesha kuwa Fomu ya kuaomba kuteuliwa kuwa mgombea itachukuliwa siku zisizopungua ishirini na sita kabla ya siku ya Uchaguzi Kif. 17 (1) na kutakiwa kuzirejesha ndani ya siku saba Kif. 17 (2).

Amesema hiyo maana yake Fomu ya uteuzi itatolewa kwa siku moja tu yaani tarehe 1 Novemba, 2024 isipokuwa unaweza kurejesha wakati wowote ndani siku saba (tarehe 1 mpaka 7).

Aidha Shaibu aliongeza kuwa Tamisemi wameshindwa kuzingatia kuwa upo uwezekano wa mgombea kuumwa au kupata tatizo litakalopelekea yeye kushindwa kwenda kuchukua Fomu siku hiyo. Intelijensia yetu inaonesha kwamba hapa ndipo mahala ambapo CCM wameweka mtego wao katika baadhi ya maeneo hasa vijijini ambako CCM wana hali ngumu wanapanga njama za kuwateka wagombea wao au kuwafanya wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kutokuwepo kwenye vituo vya kutolea Fomu kwa kuwa CCM wanazo njia za kupata Fomu hizo hata kama hawatofika vituoni.

Hivyo ametoa wito kwa TAMISEMI kuwa ni wajibu wao kijithibitisha mbele ya Umma kwamba wanaweza kusimamia Uchaguzi kwa Uwazi na Uadilifu hivyo amewataka kufanya mambi yafuatayo ambayo ni,

Kwamba kuwe na mfumo maalum wa utoaji wa taarifa zinazohusu Uchaguzi huu na kuvishirikisha vyama katika ngazi ya taifa ili visaidie kutoa ufafanuzi kwa viongozi wao wa ngazi za chini badala ya kuacha kila msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi za chini kadiri anavyotaka yeye au alivyoelekezwa na viongozi wake.

Ameongeza kuelekea siku ya kupiga Kura ili kuondosha sintofahamu zilizojitokeza wakati wa maandalizi ya kuandikisha wapiga kura, TAMISEMI ieleze ni Lini Majina ya Mawakala yanapaswa yawe yamewasilishwa kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na lini wataapishwa ili kuvipa vyama nafasi ya kujiandaa.

Kadhalika TAMISEMI iweke utaratibu rafiki wa vituo vya kuapishia Mawakala badala ya kuwataka Mawakala hao wasafiri kwa umbali mrefu kufuata kuapishwa wakati hali halisi kinachofanyika kwenda kujaza Fomu za kiapo jambo ambalo linaweza kufanyika mahala popote karibu yao bila kuathiri maana na mantiki ya kiapo hicho.
Ameitaka TAMISEMI kuacha vyama vipambane vyenyewe

Ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kuwa ACT watashiriki Uchaguzi wakipambana na watapambana tukishiriki.

Amewasihi Wananchi wajitokeze kwa wingi kwenda kujiandikisha katika daftari la Wakaazi wa Mtaa ili watumie haki yao vizuri katika Uchaguzi huu kuwachagua wawakilishi wanaowaona kuwa wataweza kusimamia maendeleo ya maeneo yao.

No comments