MUFTI MKUU SHEIKH DKT. ABUBAKAR ZUBER ATOA VYETI KWA WADAU WALIOFANIKISHA TAMASHA KUBWA LA KIMATAIFA KUHIFADHI QUAN KWA WANAWAKE
Mufti
mkuu wa Tanzania sheikh Dokta Abubakar Zuber Bin Ally ametoa vyeti vya shukrani
kwa kutambua mchango wa taasisi na wadau mbalimbali walioshiriki katika kufanikilisha
tamasha kubwa la kwanza la kimataifa la kuifadhi Quan tukufu lilofanyika katika
uwanja wa Benjamini mkapa jiji Dar es salaam.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi vyeti hivyo iliyofanyika makao makuu ya bakwata jijini
dar es salaam, alisema kwa kipekee anamshukuru Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dokta Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano aliowata ngau awali pamoja na
kuridhia ombi la kuwa mgeni rasmi siku ya mashindano.
Alisema
mheshimiwa rais pamoja majukumu mazito ya kitaifa lakini akusita kuweza kutoa
mchango wake kubwa ambao ulipelekea kufanikisha tamasha hilo kubwa la kwanza sambamba
na kukubali ombi la kuwa mgeni rasmi.
“Kipekee
ntoe shukrani kwa mheshimiwa rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa
aliotupatia kuandaa tukio hili muhimu ikiwa ni pamoja na kukubali ombi la kuwa
mgeni siku ya mashindano makubwa ya kwanza ya kimataifa ya kuhifadhi Quan
pamoja na majulumu mengi ya kitaifa aliyonayo” Alisema Mufti Dkt. Abubakar.
Katika
hatua nyingine mufti pia ameyashukuru mashirika pamoja na taasisi mbalimbali ambazo
zilishiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha kuwa mashindano hayo
ya kwanza ya kuhifadhi Quan yanafanikiwa.
Amezitaja
taasisi hizo ambazo zilikuwa sambamba na kutoa mchango kubwa katika kuhakikisha
kuwa mashindano hayo yanafanikiwa kuwa ni Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es
slaam, wakuu wa wilaya zote za mkoa wa dar es salaam, viongozi wa dini ya
kiislam kutoka ngazi mbalimbali wakiongozwa sheikh wa mkoa wa dar es salam
walid alhad.
Amezitaja
taasisi nyingine kuwa ni Taasisi za kidini, mshrikika na makampuni binafsi, mabalozi
wanaowasilisha nchi zao nchini pamoja na vyombo vya habari.
No comments