Breaking News

STEVE NYERERE WASANII TUWEKEZE KATIKA ELIMU VINGINEVYO NI KUPOTEZA MUDA TU

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, bwana Steve Mengele "Steve Nyerere" amesisitiza kuwa ili wafanikiwe katika tasnia hiyo wanatakiwa kuwekeza kwenye elimu na kulinda Utamaduni wa Kitanzania. 

Steve Nyerere amebainisha hayo leo, Julai 10, _2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutoa mrejesho wa safari yao ya mafunzo nchini Korea. 

Bosi huyo wa wasanii wa Bongo wa uigizaji nchini wakati akitoa mrejesho huo aliambatana na baadhi ya wasanii waliokwenda Korea kwaajili ya mafunzo ya kuandaa kazi zao, akiwemo Idris Sultan, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Irene Pau, Ivone Sherry "Monalisa" na wengineo.

Katika mrejesho, Steve Nyerere alisema tofauti na elimu kwa wasanii kinachotakiwa ni kuenzia Utamaduni wa Kitanzania katika kazi zao hususan katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kama wanavyofanya wakorea na katika kutumia lugha ya kwao inayofanya watambulike Dunia nzima

"Wenzetu wale wanatumia zaidi lugha yao na tamaduni zao na ndio utaratibu na Sheria za taifa hilo jambo ambalo linafanya watambulike zaidi na wamtusihi nasi tufanye hivyo ili kujitambulisha Duniani," amesema.

Pia aliongeza kuwa bodi ya filamu ya nchi imekuwa ikiwaacha huru bila ya kuwabana katika ubunifi kikubwa kinachotakiwa kuzingatia utamaduni kwa asilimia 70.

Pia amesema katika kazi zao kumekuwa na mgawanyo wa majukumu hali inayofanya kazi kuwa bora tofauti na wasanii wa Tanzania. 

Ameongeza ili kufanikiwa katika hayo wasanii, Kwa kuanzia na waandaaji, wapiga picha wanatakiwa zaidi kupata shule ili kujifunza zaidi tofauti na hivyo watakuwa wanapoteza muda kufikia malengo kimataifa.

Tofauti na hilo, Steve amesema kuwa wenzao wamekuwa na mji ambao unetengenezwa kwa ajili ya wasanii kuutumia, mfano msanii anataka kutumia nyumba, magari ama sehemu za kitalii zinapatikana katika mji huo maalumu kwaajili ya shughuli za kisanii.

Hivyo alipendekeza kwa Serikali kutenga eneo maalumu kwaajili ya wasanii kulitumia na kaomba Kwa Serikali watenge moja yaa eneo Kigamboni liwe na kil kitu litakalotumia kwa ajili ya shughuli za uigizaji. 

Steve Kwa niaba ya wasanii wote hususan fani ya uigizaji wametoa shukrani zao Kwa rais Dk Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kuwapa safari hiyo ya mafunzo na kusisitiza wataitendea haki kwa maslahi ya nchi. 

Pia aliwataka wasanii kulitumia vizuri mitandao ya kijamii katika kijiendeleza kikazi na kutukanana.

No comments