Breaking News

MBUNGE BONNAH AFUNGUKA KERO ZA WAKAZI WA KIPUNGUNI MWENEZI MAKALA AHAIDI KUZITAFUTIA UFUMBUZI

NA HERI SHAABAN (ILALA)
MBUNGE wa jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,amewasilisha malalamiko yake kuhusiana na changamoto ya muda mrefu ya wakazi wa Kipunguni kushindwa kulipwa fidia ya maeneo yao kupisha upanuzi wa Uwanja Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere. 

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli, aliwasilisha Changamoto hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Segerea  katika ziara ya Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa Amos Makala, kutembelea jimbo la segerea kuangalia uhai wa chama na kuzungumza na wanachama na kupokea kero za wananchi. 

"Mh Mwenezi wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa  tupelekee salam kwa Mwenyekiti wa ccm Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji( DMDP) ufanyike haraka barabara ziweze kujengwa changamoto za Jimbo la Segerea kwanza namshukuru Waziri wa Maji Juma Aweso ameweka mikakati ya sekta ya maji vizuri nikizubgumzia changamoto ya kulipwa fidia wananchi wa Kipawa mtaa wa Kipunguni changamoto ya muda mrefu zaidi ya miaka 27 Mawaziri wengi wamefika utatuzi wake umegonga mwamba Mh ,AMOS MAKALA tunaomba suala hili unalifahamu wakati ukiwa mkuu wa mkoa sasa tunaomba lifike hatua za mwisho baada ya Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba kufika mwaka 2023 alitoa maelekezo Wananchi watalipwa Agosti 2023 nyumba zimevunjwa na hakuna malipo yoyote mpaka sasa 2024 "alisema Bonah

Mbunge Bonnah alisema wananchi wa Kipunguni kwa sasa wanaishi katika Mahema wameshindwa kuliendeleza eneo hilo la Kipunguni na hakuna kiongozi yoyote wa Serikali anafika eneo hilo.

Akizungumzia mafanikio sekta ya afya jimbo la  Segerea linajivunia mafanikio makubwa ambayo yanafanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri alisema Serikali imejenga kituo cha afya Kinyerezi,Segerea,Kiwalani,Plani kilichopo Mnyamani na shule nyingi za Sekondari na Shule za Msingi zimejengwa.
MWENEZI wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Amos Makala, akijibu changamoto hizo madai ya Kipawa Kipunguni alimunganisha Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba akaeleza" ni kweli anafahamu changamoto ya Kipunguni yeye Mwenyewe amefika na Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli kufatilia Wizara ya Fedha ni kweli imechelewa kuwalipa wananchi wa Kipunguni na hivi Karibuni itawalipa ilikuwa Changamoto pia leo (Jana Agosti 08 /2024 amekutana na wajumbe wa Kipunguni amezungumza nao baada mwaka wa fedha Agosti 2024 malipo ya Kipunguni yatafanyika "alisema Mwigulu 

MAKALA  alisema mbunge amefatilia miaka yote lakini ameomba radhi wananchi wa Kipunguni kufuatia nchi yetu kupata changamoto za mafuriko hivyo Julai wanaweka mifumo sawa wataanza kulipwa .
 


No comments