Breaking News

BALOZI KASIKE AKOSHWA NA UTALII MUBASHARA BANDA LA MALIASILI NA UTALII SABASABA.

Balozi wa Tanzania Nchini Msumbiji CGP (Mstaafu). Phaustine  Kasike ametembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye Maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara sabasaba Dar es Salaam  na kujionea namna ambavyo Hifadhi ya Ngorongoro inaonyesha vivutio vya utalii mubashara kutoka Ngorongoro.

Balozi Kasike ni miongoni mwa maelefu ya wananchi waliotembelea banda hilo na kupongeza ubunifu uliofanywa na Wizara hiyo kupitia mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kutangaza vivutio vya utalii kwa kuwaonesha wananchi mubashara matukio yanayotokea hifadhini hali inayoongeza hamasa ya wananchi wanaoendelea kutembelea banda hilo.

Programu ya kuonesha matukio ya utalii mubashara kutokea Ngorongoro itaendelea katika banda la wizara ya maliasili na utalii hadi tamati ya maonesho hayo tarehe 13 Julai, 2024.
 

No comments