Breaking News

WAZIRI MAVUNDE AMWAGIZA KAMISHNA WA MADINI KUUNDA TIMU KUFANYA UKAGUZI KAHAMA

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akiwa na watendaji wa Wizara ya Madini na Viongozi wa Nkandi Gold Mine wa Wilayani Kahama-Shinyanga kwenye kikao cha usuluhishi baina  ya wamiliki wa duara Na. 7 na 8.

Katika kikao hicho, Waziri Mavunde amemwagiza Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrahman Mwanga kutuma Timu kukagua usalama wa shughuli za uchimbaji katika maduara hayo kabla hajatoa uamuzi wa mwisho wa kutatua mgogoro wa muingiliano uliopo baina ya wamiliki wa maduara hayo.