Breaking News

KAMATI YA MAFUNZO MAHAKAMA YA RUFANI YAPITISHA RASIMU YA MPANGO WA MAFUNZO

Katibu wa Kamati ya Mpango wa Mafunzo wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bw. Victor Kategere (kulia), ambaye pia ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, akitoa Reno la utangulizi katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Maktaba ya Mahakama ya Rufani. (katikati) ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Augustine Mwarija ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, na (kushoto) ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. George Herbert.
Mwenyekiti wa Kamati Mpango wa Mafunzo wa Mahakama ya Rufani Mhe. Augustine Mwarija ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani  Tanzania(katikati) akiongoza wajumbe wa kamati hiyo cha  kupitia rasimu ya mpango wa mafunzo wa Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2024/2025
Mwenyekiti wa Kamati Mpango wa Mafunzo wa Mahakama ya Rufani Mhe. Augustine Mwarija ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania (katikati) akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bi. Judith Mrema akiwasilisha rasimu ya mpango huo. Picha zote na Magreth Kinabo- Mahakama

Na: Tawan Salum
Mahakama ya Rufani ya Tanzania imepitisha rasimu ya   mpango mafunzo ili kuweza kuwajengea uwezo wa utendaji wa kazi wa wafanyakazi wake kwa kuwapangia mpango maalum wa mafunzo wa muda mfupi na mrefu kwa mwaka 2024-2025.

Akizungumza katika kikao maalum cha Kamati ya Mpango wa Mafunzo, kilichofanyika katika ukumbi wa Maktaba Mahakama ya Rufani  leo tarehe 25 Juni ,2024 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Mafunzo ya Mahakama ya Rufani Mhe. Augustine Mwarija ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani  Tanzania, alisema kuwa kazi  kubwa  ya kamati ni kumshauri Jaji Mkuu, Mtendaji Mkuu wa Mahakama pamoja na Msajili wa Mhakama ya Rufani namna bora ya utekelezaji wa mpango huo.

“Tumeshapiga hatua na utekelezaji umehusisha kada zote mahitaji yameoneshwa ili kuweka mambo sawa yatakayosaidia mafunzo kufanyika katika kada zote ili hatimaye kuleta ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa Mahakama ya Rufani na Taifa kwa ujumla. Hivyo kazi yetu sisi ni kushauri na kusubiri utekelezaji wake.” alisema Mhe. Jaji Mwarija. 

Aliongeza pia mafunzo hayo watakayopatiwa wafanyakazi hao, likiwemo  utamadani wa  Mahakama hasa kutunza siri za waadawa kutozizungumza kwa kwa watu wasiostahili kwani inaweza kuleta taharuki  kubwa kwenye jamii yetu kwa ujumla, mara nyingi Mahakama imekuwa ikisemwa kwenye vyombo vya habari lakini namna bora ya kuwajibu ni kukaa kimnya na kuwajibu kwa vitendo katika utendaji wetu wa kazi.

Naye Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bw. Victor Kategere alisema kuwa katika mkakati wa mafunzo hayo wataweka pia namana bora ya kuwa na urithishaji wa viongozi (succession plan) kwa kuwa itasaidia katika kuwajua na kuwaandaa viongozi watakaokuja kuongoza baada ya walipo madarakani kuondoka kwa kustaafu ama kufariki. Pia utasaidia  kuboresha utendaji wa kazi ndani ya Mahakama ya Tanzania.

Naye Mjumbe wa kamati hiyo, ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Rufani Mhe. George Herbert alisema kuwa mpango huo, ni mzuri na utaleta tija na ufanisi katika kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Mahakama hiyo na kurahisisha utendaji wa kazi kuwa rahisi na wenye weledi.