Breaking News

KIIZA MAYEYE: BAJETI AIENDI KUJIBU CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Waziri Kivuli wa Fedha, Mipango na Hifadhi ya Jimii Bi. kiza Mayeye akifafanua jambo wakati akichambua bajeti ya serikali 2023/24 makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Waziri Kivuli wa Fedha, Mipango na Hifadhi ya Jamii Bi. Kiza Mayeye amesema Bajeti ya ya Serikali iliyowasilishwa Bungeni Juni 13, mwaka huu, haileti majibu ya changamoto ya ukosefu wa ajira unaolikabili kundi kubwa la vijana, haitoi majibu juu ya maumivu ya kupunjwa mafao kwa wastaafu, pamoja na kushindwa kutoa suluhisho juu ya maumivu ya wananchi kukosa huduma za matibabu na mfumuko wa bei ya bidhaa mbalimbali inayoendelea kuwa juu kila wakati.

Akizungumza wakati akifanya Uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali mwaka wa fedha 2024/25 amesema katika bajeti hiyo Shilingi trilioni 49 zinazotarajiwa kutumika katika mwaka wa fedha 2024/25 watawala wameweka matumizi yao kuwa shilingi Trilioni 34.6, huku shughuli za maendeleo yanayowagusa wananchi zikitengewa kiasi cha shilingi Trilioni 14.75 tu.

Alisema kwa mujibu wa bajeti hiyo ambayo inaenda kulipa gharama kubwa ya matumizi ya anasa kwa watawala na kuliacha kundi kubwa la wananchi likielea katika ufukara uliopitiliza.

"Kwa mujibu wa bajeti ambayo iliyowasilishwa bungeni June 13 inaonyesha wazi kushindwa kujibu changamoto za wananchi hususani ukosefu wa ajira unaolikabili kundi kubwa la vijana, haitoi majibu juu ya maumivu ya kupunjwa mafao kwa wastaafu, pamoja na kushindwa kutoa suluhisho juu ya maumivu ya wananchi kukosa huduma za msingi ikiwemo matibabu pamoja na mfumuko wa bei" Alisema Bi Mayeye.

Alisema tangu kuingia madarakani serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan deni la taifa limekuwa likikuwa kwa kasi kubwa hali inayotishia maendeleo ya watu na uwezo wa nchi kujihudumia.

Akizungumzia upande wa eneo la matumizi ya gesi asilia Ndg Mayeye amesema Serikali imeamua kuinyonga sekta hiyo kwa kuweka kodi Shilingi 382 kwa kilogramu moja hali inayoenda kuua ari ya watumiaji kutokana kuongezeka kwa gharama.

"Bajeti haiendi kujibu changamoto za Wananchi, bali inakwenda kulipa gharama kubwa ya matumizi ya anasa kwa watawala na kuliacha kundi kubwa la watu likielea kwenye ufukara wa kutupwa." Alisema Bi Mayeye.