Breaking News

DKT. BITEKO KUFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA KITAALUMA LA UCHUMI WA BULUU

Naibu waziri mkuu na waiziri wa nishati na mhe. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano kitaaluma la tatu la uchumi wa Blue litakalofanyika tarehe 4 na 5 Julai katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Akizungumzia juu ya maandalizi ya kongamano hilo mkuu wa chuo bahari, Dokta Tumaini Gurumo amesema lengo la kongamano hilo la kitaaluma ni kuwaleta pamoja wanataaluma kutoka nchi 11 kwa lengo la kuijendea uelewa kwa jamii kuhusu faida na mchango wa Sekta ya Bahari.

"Katika siku mbili za kongamano hili washiriki kutoka ndani na nje ya nchi watapata wasaa wa kuzungumza na kujadiliania juu ya mafanikio ya uchumi wa bluu pamoja na changamoto zilizopo kufikia malengo ya teknolojia kwa ukuaji wa uchumi wa buluu". Alisema Bi. 

Alisema katika kongamano hilo wanataaluma pia watawasilisha tafiti mbalimbali walizofanya za kijeojorojia na utunzaji wa mazingira 
na kujadiliwa na washiriki kwa lengo la kutoa picha halisi kwa manufaa ya nchi.

Kongamano la mwaka huu limeandaliwa na chuo cha bahari Dar es salaam (DMI) kwa kushirikiana na Chuo cha bahari cha Ghana na kubeba kauli mbiu isemayo "Kuiendea kesho Kujumuisha  Ulinzi na Usalama wa Majini, Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na Maendeleo ya Teknolojia Kwa Ukuaji wa Uchumi wa Buluu".